Michezo

Majina 10 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia yatangazwa, Neymar akalia kuti kavu

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina 10 ya wachezaji wa kiume wanaowania tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka 2017/18.

Image result for Messi Ronaldo and mbappe
Ronaldo, Mbappe na Lionel Messi

Kitu cha kushangaza kwenye orodha hiyo jina la Neymar na Pogba ambao mwaka jana waliingia kwenye orodha hiyo mwaka huu hawajafanikiwa kuingia.

Orodha ya majina hayo ni Cristiano Ronaldo (Juventus), Kevin De Bruyne (Man City), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Eden Hazard (Chelsea), Harry Kane (Spurs), Kylian Mbappe (PSG), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Mohamed Salah (Liverpool) na Raphael Varane (Real Madrid) .

Majina haya yamechujwa kuanzia tarehe 3 Julai 2017 hadi Julai 15, 2018 na tuzo zitatolewa mwezi Septemba 24, 2018 jijini London Uingereza.

Related Articles

8 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents