Habari

Majina ya wabunge 8 wapya walioteuliwa CUF sio mapya – Prof. Lipumba

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa majina ya Wabunge 8 wapya wa Viti Maalum wa CUF walioteuliwa sio mapya yalipelekwa na Maalim Seif ofisi za NEC mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam, Prof. Lipumba amesema majina ya wabunge 8 wapya wa viti maalum wa CUF walioteuliwa sio mapya na kwamba yalipelekwa na Maalim Seif ofisi za NEC.

“Majina yaliyotangazwa ya Viti Maalum ya wale ambao tuliwavua Uanachama majina hayo yanatokana na orodha iliyopelekwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kwenye Tume ya Uchaguzi hakuna majina mapya ambayo yaliteuliwa nje ya orodha ile hii ndio orodha ambayo tumeizingatia,” amesema Prof. Lipumba.

“Kwasababu orodha ya uchaguzi majina unapeleka kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika alafu wao wanateua kutoka orodha hiyo pakitokea nafasi ya viti maalum ndio ileile orodha iliyopelekwa kabla ya uchaguzi mkuu ndio inayotumiwa kujaza nafasi hizo vyama vinapata fursa ya kupata mapendekezo kutokana na orodha ile kwasababu ya Tume ya uchaguzi haiwezi ikajua vipaumbele vya chama na wote walio kwenye orodha ile kwahiyo walioko kwenye orodha tumeinawajibika kukiuliza chama.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents