Michezo

Majina ya wanaowania tuzo za VPL msimu 2017/18 haya hapa

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini limetangaza majina ya wanaowania tuzo za ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18 zinazo tarajiwa kufanyika Juni 23,2018 kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kila unapomalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania kumekuwa na utaratibu wa kutolewa kwa tuzo mbalimbali ikiwemo ya mchezaji bora wa VPL huku tuzo ya mchezaji wa kigeni ikiondolewa mwaka huu na hivyo kutoa fursa kwa watu wote kuwania moja.
TFF imesema kuwa msimu huu imeongeza tuzo ya mwwamuzi bora msaidizi ambayo haikuwepo hapo awali ikiwa na lengo la kuthamini nafasi na mchango wa waamuzi wasaidizi.
Tuzo zitakazo tolewa ni za Bingwa, Mshindi wa pili, Mshindi tatu, Wanne, Mfungaji bora, timu yenye nidhamu, ‘Under twenty player’, mchezaji bora chipukizi, Mwamuzi bora msaidizi, Mwamuzi bora, Kipa bora na kocha bora, Goli bora, ‘Vpl best eleve’ , Mchezaji wa heshima wakati zawadi zikitarajiwa kutangazwa siku za usoni.
Kamati ya tuzo ya TFF imekamilisha orodha ya wachezaji 30 watakao wania tuzo hizomsimu huu wa mwaka 2017/18.
Kwenye majina ya wachezaji 30 waliyo orodheshwa kuwania tuzo hizo watachujwa mpaka kufikia 10 kisha watatu na kutafuta mshindi.
1. Habibu Kyombo (Mbao)
2. Khamis Mcha- Ruvu Shooting
3. Yahya Zayd-Azam
4. Razack Abalora-Azam
5. Bruce  Kangwa-Azam
6. Aggrey Morris -Azam
7. Himid Mao –Azam FC
8. Awesu Awesu –Mwadui
9. Adam Salamba-Lipuli
10. Mohammed Rashid-Prisons
11. Shafiq Batambuze-Singida
12. Mudathir Yahya-Singida United
13. Marcel Kaheza- Majimaji
14. Ditram Nchimbi-Njombe Mji
15. Eliud Ambokile- Mbeya City
16. Shaaban Nditi-Mtibwa
17. Tafadzwa Kutinyu-Singida
18. Ibrahim Ajibu- Yanga
19. Gadiel Michael-Yanga
20. Papy Tshishimbi-Yanga
21. Kelvin Yondani-Yanga
22. Obrey Chirwa-Yanga
23. Aishi Manula-Simba
24. Emmanuel Okwi-Simba
25. John Bocco-Simba
26. Jonas Mkude-Simba
27. Erasto Nyoni-Simba
28. Shiza Kichuya-Simba
29. Asante Kwasi –Simba
30. Hassan Dilunga-Mtibwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents