Burudani

Majina ya wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye BET 2017 yatajwa

By  | 

Majina mengine ya wasanii wanaotarajiwa kuwasha moto kwa kutumbuiza kwenye jukwaa la tuzo za BET kwa mwaka huu yametajwa.

Wasanii waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Chris Brown, Lil Wayne, DJ Khaled, Big Sean, Post Malone, Roman GianArthur, na Jessie Reyez.

Wasanii hao wataungana na wengine ambao walitajwa mwanzo kutumbuiza siku hiyo akiwemo Bruno Mars, Future, Migos, Trey Songz, Tamar Braxton. Wakati huo huo mchekeshaji Leslie Jones anatarajiwa kuwa mtangazaji kwenye tuzo za mwaka huu.

Tuzo hizo zitafanyika Juni 25 kwenye ukumbi wa Microsoft Theater uliopo mjini Los Angeles, Marekani.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments