Habari

Majonzi vilio vyatawala baada ya kuwasili mwili wa marehemu Pancho kijijini kwao Gairo (+Video)

Mara tu baada ya mwili kuwasili

Usiku wa kuamkia leo mwili wa aliyekuwa mwandaaji wa muziki (Producer) katika studio za B hits Pancho Latino uliwasili katika kijiji alichozaliwa cha Msingisi Gairo mkoani Morogoro. Mwili huo umewasili usiku ukitokea DarĀ  es salaam sehemu ambayo alikuwa akifanyia kazi zake ambako ndio mauti yalimkuta siku ya jumanne maeneo ya Mbudya.

Siku ya jana asubuhi mwili huo uliagwa katika hospitali ya Lugalo kabla ya kuelekea mkoani Morogoro ambako ndio ataenda kuhifadhiwa huko,baada ya mwili huo kuwasili Gairo majonzi simanzi na vilio vilitawala nyumbani kwao baada ya kuwasili kwa mwili huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu Pancho mahala pema peponi “AMEEN”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents