Mitindo

Makala- AR 2013 Enchanted Iwe Chachu Ya Wadhamini

Ally Rehmtullah

Na Orvin Sanga.

Karibuni, mbunifu mahiri wa Kitanzania Ally Remtullah alifanya shoo yake mahususi kabisa katika kusherehekea uwepo wake katika tasnia ya ubunifu, mitindo na mavazi kwa kipindi cha miaka 5 iliyopewa jina la Ally Remtulla 2013 Enchanted Jungle.

Kwa ufupi shoo hiyo imekua moja kati ya shoo zilizoandaliwa kwa kiwango cha juu kabisa kuanzia mipango, uchaguzi wa eneo lilipofanyika tukio lenyewe, burudani ya muziki pamoja na ubunifu wa mandhari ya eneo lote kwa ujumla pamoja na mtiririko wa tukio lenyewe kutoa taswira tatu tofauti.

Lakini hii ya Ally Remtullah imekwenda kuingia katika viwango vya ‘Premium Event’ na kuleta changamoto mpya kwa waandaji wa matukio ya kisanaa na burudani yanayokuja. Tulishazoea matukio makubwa ya kijamii kama Kilimanjaro Music Awards, Swahili Fashion na Miss Tanzania na hii imeonyesha uwezekano wa premium events kua hata kwa show ya mbunifu mmoja.

Ninachopenda kujadili leo ni kwamba uandaaji wa matukio ya namna hii yasiishie kwa makampuni kubagua bali yaangalie ni namna gani wanaweza wakaboresha mazingira hasa hasa mazingira ya udhamini ambapo yatapanua wigo wa ubunifu katika uandaaji matamasha kwani kwa udhamini ambao umeonekana kwa Ally Remtullah nina uhakika kati ya waliokuwemo katika shoo ile walipata mawazo wa namna wanaweza kuboresha matukio yao katika siku zijazo.

Si kama najaribu kuwasemea watu ama kujaribu kuwaombea huruma lakini ili Tanzania ipige hatua lazima wadau wote watoe ushirikiano kwa wahusika wa tasnia hizo ili maendeleo yawe ya tasnia yote na si kwa mtu mmoja mmoja wa tasnia hizo. Tunahitaji kuzoea aina hizi viwango za matukio ili kuwapa msukumo wadau wengine ambao bado wanatafakari ni vipi watajihusisha na matukio hayo kwa siku za baadae.

Mfano ni namna ambavyo event nyingi zilizokuwa na mwelekeo wa kuwa event kubwa zimekufa baada ya sapoti kupotea badala ya kujitokeza kwenda kuzi sapoti. Ki mtazamo wa kawaida, kama udhamini wa makampuni kama Mercedes Benz na Dulux Paints ambao wao hawakuwa wakijihusisha zaidi na event za namna hiyo, ingawaje kampuni za brand hiyo hiyo zimekuwa zikidhamini matukio ya aina hiyo kwenye nchi kama Afrika Kusini na Marekani zimejitokeza basi ni nafasi ya makampuni mengine kujitolea kusapoti event hizo na kuwapa raha watanzania.

Tulishazoea Makampuni ya vinywaji moto na baridi, sigara na za simu tuu kama TBL, Serengeti, Coca Cola, Vodacom, Airtel, na TCC, kuwa mstari wa mbele katika kudhamini matukio yenye mrengo wa kisanaa na zenye ubora wa juu.

lakini kwa sasa ukiachilia TCC ambao wao wamekuwa wakifanya vizuri zaidi wengine wameshuka kiwango kwa kupunguza udhamini ama kwa kudhamini matamasha kwa kiwango ambacho si mazoea ya watanzania.

Mathalani ukienda hata nje ya nchi na kukutana na wadau wengine, iwe Zambia, Kenya, Uganda, Rwanda Afrika Kusini wote watakutajia moja kati ya kampuni ambazo nilikuandikia hapo juu kwamba wakitaka kushirikiana na mtu yeyote Tanzania basi ikifika kwenye udhamini watakutajia moja ya kampuni hizo, hivyo ujio wa kampuni kama Dulux na Mercedes Benz uwe njia ya makapuni mengine ambayo mara nyingi huweka utetezi wa kisera katika kubagua aina ya udhamini wanaotoa uwe chachu ya kurudisha hadhi iliyoanza kupoteza.

Ukiangalia kwa makini utapata pia kujiuliza kwa nini Kampuni ambazo zimekuwa zimepata hadhi ya kuwa kama brand ( chapa) bora hazionyeshi ubora wake kwenye matukio ya kiburudai mara kwa mara lakini wamekuwa wepesi kwenye matukio yanayohusu mwelekeo wa kisiasa ingawaje fursa inayopatikana katika tukio kama la Ally Remtullah 2013 enchanted Jungle kibiashara ni kubwa kama ilivyojionyesha kwa aina za kada zilizohudhuria onyesho hilo.

Kampuni kama CRDB, NMB, BARCLAYS, hazijitokezi mara kwa mara, wakati ukiangalia muundo wa shughuli yenyewe unaona kabisa walistahili kabisa kuwepo lakini wanakwazwa na mipango ya kisera
Nilipoongea na Ally wiki moja kabla ya event hiyo alisema yeye ametumia mwaka mmoja kuandaa shoo hiyo tangu mwaka jana na kwamba alijaribu kuomba udhamini sehemu nyingi lakini zilizojitokeza kufanikisha ni hizo tulizoziona matangazo yao yakiwa katika eneo la tukio.

Inaonekana Ally Remtullah alielewa ni namna gani anahitaji kujipanga kwa ajili ya kuwasilisha event nzuri kwa wanajamii hivyo kujipanga.
Tukiwa kama wadau wa sanaa na burudani tunapenda kutoa Kudos kwa Ally Remtullah na wote walioshiriki kufanikisha sherehe hiyo kwa kiwango kilichoonekana .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents