Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Makala: Bongo Fleva na ‘kampa, kampa tena’ (+Video)

Kupitia Bongo5 nakuletea wasanii kadhaa wa Bongo Fleva waliofanya kazi zaidi ya moja, yaani msanii kamshirisha mwenzake kwenye ngoma yake, kisha baadaye akaja kumshirikisha msanii huyo huyo ila kwenye ngoma nyingine tofauti.

Kwa lugha ya mtaani isiyo rasmi tunaweza kusema ‘kampa, kampa tena’, ila hawa ni wale wasanii wasio katika kundi moja la kimuziki, lebo au umoja wowote ule.

 1. Izzo Bizness, Shaa & Barnaba

Izzo aliwahi kuwakutanisha wakali hawa kwenye ngoma moja ambayo ilitamba sana kwenye Bongo Fleva, ngoma ni ‘Love Me’ ambayo mwishoni ndipo inasikika sauti ya Shaa.

Achilia mbali kazi hiyo Izzo  anakuja kufanya kazi nyingine na Shaa aliyoipa jina la ‘Kidawa’ ambayo nayo pia ilifanya vizuri. Izzo anaamua kuwakutanisha wote tena kwa pamoja kwenye ngoma yake ya ‘Usijioverdose’ ambayo pia ilifanya vizuri.

2. Damian Soul na Joh Makini

Mkali huyu ambaye anaaminika kuwa na sauti ya kipekee sana kwenye Bongo Fleva alifanya kazi ya kwanza na Joh Makini iliyokwenda kwa jina la ‘Ni Penzi’ ambayo ilifanya jina Damian Soul kuwa kubwa.

Akamua kuchovya asali kwa mara ya pili kwa kumpa tena shavu Joh Makini kwenye ngoma yake ya ‘Baraka’ iliyopikwa na Pancho Latino pamoja na Hermy B kutoka B’hits.

3. Shetta na Diamond Platnumz

Ngoma ya ‘Nidanganye’ waliofanya pamoja ilimpa jina kubwa na kumbadilisha kabisa Shetta kimuziki, achili hilo mbali pia ilimpa Shetta  nafasi ya kuwania tuzo za KTMA kwa wakati ule.

https://youtu.be/1oiqIkHmaNk

Shetta alimua kufanya na Diamond kazi nyingine aliyoipa jina la ‘Kerewa’ lakini hii ilikuwa na utofauti kidogo na ile ya mwanzo, kwani aliwekeza fedha nyingi kuitangaza kwenye video waliyoifanyia Afrika Kusini.

4. Bill Nas na T. I. D

Hawa wote walikuwa wakifanya kazi chini ya usimamizi wa Radar Entertainment pamoja na Jordan na vipaji vingine. Kolabo yao ya kwanza ni ile ijulikayo kama ‘Raha’ ambayo pia walimpa shavu Nazizi kutoka nchini Kenya.

Baada ya ngoma ya mwanzo kufanya vizuri Bill Nas alimshirikisha tena T. I. D kwenye ngoma  yake ya ‘Ligi Ndogo’, ni wazi na yeye alinogewa kufanya kazi na Mzee kigogo.

5. Linex na Diamond Platnumz

Wimbo wa mwanzo waliutoa kitambo kidogo ambao ni ‘Nitaificha Wapi’, kitambo hicho wote wawili muziki wao ulikuwa wa kiwango za kawaida ukilinganisha na sasa ambapo Diamond amepiga hatua zaidi.

Wakati Diamond ameanza kupata mafanikio katika ngazi za kimtaifa, Linex aliona ni wakati muhafaka wa kufanya kazi nyingine na Diamond kama njia ya yeye ‘kujipush’ kuelekea kimataifa zaidi.

Wakatoa wimbo uitwao Salima ambayo Linex aliamini ingemtangaza kimataifa, lakini baadae akaja kudai utengenezaji wa video ilikwamisha hilo kitu kilicholeta mgogoro kati yake na director Adam Juma.

6. Tunda Man na Alikiba

Ni vigumu sana kwa wasanii wanaofanya muziki wa aina moja kufanya kazi kwa pamoja mara kwaa mara, hasa kwa wasanii wanaoimba ila hawa waliweza hilo.

Tunda Man alimshirikisha Alikiba kwenye ngoma yake ya ‘Starehe Gharama’ ambayo pia alikuwepo Chege mkali kutoka TMK, na huo ukawa mwanzo wa safari.

Safari ya kolabo ikaendelea pale Tunda Man alipokuja kumshirikisha tena Alikiba kwenye ngoma ilyokwenda kwa jina la ‘Msambinunga’ iliyosimamiwa na prodyuza Shedy Clever.

7. Nay wa Mitego na Diamond Platnumz

Nay Wamitego alimshirikisha mkali huyu kutoka WCB kwenye ngoma yake ya ‘Muziki gani’ ambayo ilifanya vizuri sana na kumuongezea Nay wa Mitego mashabiki wengi.

Nay wa Mitego akaona isiwe tabu, akaja kumshikisha tena Diamond kwenye ngoma yake ya ‘Mapenzi au Pesa’ ambayo nayo ilifanya vizuri kwa kiasi fulani ingawa video yake hadi leo haijatoka.

 

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW