MakalaUncategorized

MAKALA: Fahamu utofauti uliyopo kati ya VEVO na YouTube

Kumekuwa na maswali katika mitandao ya kijamii hususani hapa Tanzania kuhusu msanii kutumia akaunti ya VEVO au ya YouTube huku wengi wakienda mbali kuwa YouTube kuna ujanja mwingi kuliko VEVO kuanzia mfumo wake wa kupata views.

Hapa chini nimeorodhesha vitu ambavyo bila shaka vitakusaidia kuelewa utofauti uliopo na jinsi mitandao hii inavyofanya kazi.

Umiliki

Website ya YouTube imeanzishwa mwaka 2005 na mmiliki wake ni kampuni ya Google wakati website VEVO imeanzishwa mwaka 2009 na inamilikiwa na Sony Music Entertainment, Universal Music Group na Abu Dhabi Media.

Je, ukiwa Tanzania unaweza kuingia VEVO kama unavyoingia YouTube?

Ukweli ni kwamba hauwezi kuingia moja kwa moja kwenye website ya VEVO (vevo.com) kama unavoingia kwenye website ya YouTube (youtube.com). Hii ni kwa sababu vevo haijaanza kufanya kazi Tanzania wakati YouTube inapatikana karibia nchi zote duniani labda zile ambazo serikali imezuia mtandao huo kwa sasa vevo inafanya kazi nch i 20 tu duniani nazo ni Australia, Brazil, Canada, China,Ufaransa, Germany, India, Ireland, Italia,Japani, Mexico, Uholanzi, New Zealand, Poland, Korea Kusini,Hispania, Thailand, Uingereza na Marekani.

Je, ni watu gani wanaotumia mitandao hii mikubwa duniani?

Mtandao wa YouTube kwa sasa unatumiwa na kila mtu (Wasanii, Makampuni, na Wafanyabiashara) na kujiunga ni rahisi ili mradi uwe na barua pepe ya G-mail lakini ni tofauti na VEVO ambapo ni Wasanii/Wanamuziki pekee ndio wanatumia mtandao huo kwa kuweka kazi zao hivyo usitarajie kuingia kwenye mtandao wa VEVO na kukuta video za vichekesho au video za maelekezo kama ilivyo YouTube.

Faida na hasara ya msanii kutumia akaunti ya VEVO au YouTube.

Kwanza kaa ukijua kuwa YouTube ndio mtandao mkubwa na wenye watu wengi duniani kuliko VEVO na ndiyo maana VEVO wakachukua uamuzi wa kufanya kazi pamoja na Youtube mwaka 2010 baada ya kugundua kuwa wangeendelea kufanya kazi kivyao basi wangekuwa na watazamaji wachache.

Kwa hiyo kabla ya kuangalia uzuri wa msanii kujiunga na VEVO inakupasa uelewe hilo kuwa kusingelikuwepo kwa makubaliano ya kibiashara kati ya YouTube na VEVO basi mtandao unaoitwa VEVO usingepata hata umaarufu tunaouzungumzia leo. Kwa hiyo mtandao wa VEVO ulijiunga na YouTube kwa makubaliano ya kibiashara, na hii ndiyo maana hata VEVO wenyewe wana akaunti yao ndani ya mtandao wa YouTube.

1-Faida ya msanii kuwa VEVO ni kwamba atasaidiwa nyimbo zake kupigwa promo na VEVO wenyewe kwa sababu hao wapo kibiashara zaidi wakati YouTube hawafanyi hivyo badala yake msanii anategemea ukubwa wa mashabiki wake yaani (Subscribers).

2-VEVO wanabana uhuru wa msanii wa kuposti videos ambazo sio rasmi kama matamasha yao au hata video za behind The Scene hao wanataka (Official Release Videos) wakati kwenye mtandao wa YouTube msanii anakuwa huru kuposti videos zozote alizorekodi ilimradi zisivunje sheria zilizowekwa na YouTube. Na hapa ndio maana kuna baadhi ya wasanii wanaotumia akaunti za VEVO wanalazimika kuwa na akaunti mbili yaani akaunti ya Youtube na VEVO ili wapate uhuru wa kuposti matukio mbalimbali . Mfano Lady Gaga, Diamond Platnumz nk.

3-Faida nyingine ya kutumia VEVO ni kwamba inasaidia msanii kutafutwa kwa urahisi na mashabiki wake hususani youtube pale unapotafuta kazi za Msanii husika au jina lake.

4-Malipo ya mtandao wa VEVO ni makubwa ukilinganisha na YouTube hii ni kwa sababu akaunti za wasanii wengi za VEVO zipo chini ya makampuni au lebo za muziki zinazowasimamia wakati YouTube hao wanalipa msanii kadri ya matangazo yanavyozidi kucheza kwenye channel yake hakuna makubaliano rasmi ya malipo.

5-Usimamiaji wa akaunti za VEVO na YouTube. YouTube channel zake zinaongozwa na mtumiaji mwenyewe lakini akaunti za VEVO zinafunguliwa na kuongozwa na watu maalumu kutoka VEVO, hivyo msanii hatakuwa huru kukagua akaunti bali atakuwa anapata notifications tu kutoka VEVO.

Je, wasanii wa Afrika wanatumia mtandao wa VEVO kupata views?

Hapana wasanii wa Afrika na nchi nyingine ambako VEVO haipatikani na wamefungua akaunti za VEVO hupata views kupitia YouTube na sio VEVO hii ni kwa sababu akaunti zao za VEVO zipo ndani ya YouTube.

Kiufupi VEVO inapata views wengi kutoka kwenye mtandao wa Youtube duniani hii ni kutokana na ushirikiano wake wa kibiashara kuliko hata views wanaopatikana moja kwa moja kutoka kwenye mtandao wa VEVO yaani (vevo.com)

Je, msanii anaweza kununua Views YouTube au VEVO?

Ukweli ni kwamba kuna uwezekano wa kununua views kwenye mtandao wa YouTube ila kwa zile akaunti ambazo hazioneshi matangazo na kitendo hicho endapo kitafanywa na akaunti zilizounganishwa na matangazo (Google Adsense) upo uwezekano akaunti husika kufutwa. Mchezo huu kwa akaunti za VEVO hakuna kabisa kwani zinaongozwa na wenyewe VEVO.

SOMA ZAIDI- Ommy Dimpoz adai kuna baadhi ya wasanii wananunua views YouTube

Ni kweli VEVO inatumiwa na wasanii maarufu pekee?

Hapana, VEVO inatumiwa na kila msanii/Mwanamuziki kinachohitajika ni kufuata utaratibu wa kujisajili. Kuna wasanii wakubwa hawatumii VEVO wapo YouTube na kuna wasanii wengine wadogo wapo YouTube, Kwa sasa wasanii ambao wanatumia akaunti za VEVO hapa Tanzania ni Diamond Platnumz, Alikiba, Jux,  Gosby, Grace Matata, nk.

Kwa hiyo VEVO ni mtandao unaojitegemea ila upo ndani ya Youtube kama Partnership kibiashara na mamilioni ya views kwenye video za VEVO yanatoka YouTube.

Kwa hiyo kama VEVO ikijitoa kwenye biashara na YouTube basi mtandao huo utakuwa na watazamaji wachache mno duniani kwani hata nchi ambako mtandao wa VEVO unapatikana bado mtandao wa YouTube una watumiaji wengi na hata VEVO muda mwingine hutumia mtandao huo kupromoti kazi za wasanii wao.

Kwa wepesi ni kwamba website ya VEVO ipo syndicated kwenye website YouTube ili kufanya kazi kiurahisi kwa nchi ambazo VEVO haipatikani.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents