Makala

MAKALA: Kutoka kwa mashabiki “Alikiba unakua kiumri kimuziki unadumaa, badilika utapotea”

Wahenga walisema muda ni ukuta hauwezi kushindana nao, na hii inakuja kujionesha hata katika maisha ya kawaida kadri muda unavyozidi kwenda vitu kama mitindo, teknolojia na hata ladha ya muziki nayo inabadilika, lakini sio kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, King Kiba.

Related image

Alikiba bado anaamini kuwa nyimbo zake za zamani alizowahi kuziachia iwe kwa kuvujisha au kuziachia mtandaoni, kwa muda huo zinaweza kutumika tena na ku-hit jambo ambalo sio baya kwa msanii lakini kwa mtu mkubwa kama Alikiba huo ni uvivu.

Hebu turudi nyuma kidogo, Alikiba kwa miaka mingi alikuwa kimya kwenye muziki lakini mwaka 2014 aliporudi kwenye gemu na kuanza kutoa nyimbo kama Mwana (2014), Chekecha Cheketua (2015), Aje (2016), Seduce Me (2017) na Nagharamia watu wengi walianza kumuelewa na aliongeza mashabiki wapya ambao kwa miaka 2006 wakati anafanya vizuri wengi walikuwa ni wadogo kiumri.

Kutokana na ukubwa wa nyimbo hizo alizoachia kwa miaka mitatu mashabiki wengi wapya walianza kumfuatilia na kuamini kuwa wapo upande sahihi, lakini sio kwa mwaka 2018.

Kwa mwaka huu 2018 Alikiba umewakosea mashabiki wako wapya na hata baadhi ya mashabiki wako wa zamani, kwani nyimbo zote tatu hakuwa wimbo uliopokelewa vizuri kama zile ulizoachia miaka mitatu ya nyuma.

Wimbo kama Mvumo wa Radi sidhani kama unaweza ukaufananisha na Mwana, au wimbo kama Maumivu Per Day unaweza ukaufananisha na Aje au pengine wimbo wake mpya wa Hela unaweza ukaufananisha na Seduce Me.

Hii ni ishara tosha Alikiba kwa mwaka huu umewaangusha mashabiki wako, ngoma zote ulizotoa zimepokelewa kawaida sana.

Na, pengine huenda asiwe yeye peke yake aliyetoa nyimbo za kawaida kwa mwaka huu lakini, tunakuzungumzia yeye kutokana na ukubwa wa jina lake ‘KING KIBA’.

Achilia mbali, mashabiki wengi wa Alikiba ni wakubwa kimri kuanzia miaka 25 na kuendelea, lakini hiyo isimfanye Alikiba kubweteka na kutoa nyimbo za kawaida kama Mvumo wa Radi, Hela na Maumivu per Day.

Nyimbo kama Hela na Maumivu Per Day zote Alikiba alishawahi kuziachia mtandaoni miaka ya nyuma na zimesikilizwa hadi watu wakazichoka, sasa ni uvivu gani hadi akaamua kuziachia tena ile hali anajua muziki wa sasa unahitaji ubunifu wa hali ya juu ili usikilizwe zaidi.

Alikiba ni msanii mwenye kila sifa ya kuitwa msanii mkubwa, anauwezo wa kuandika nyimbo na kabarikiwa sauti, sasa ni kitu gani kinachomfanya mpaka arudie nyimbo kama Maumivu Per Day na Hii aliyoichia leo ya Hela? bila shaka ni uvivu.

Kwa jinsi muziki wa sasa ulivyo kiushindani, Alikiba usitegemee mashabiki wako wapya watashindwa kukushambulia endapo utaendelea kutowatendea haki kwa kuachia nyimbo za kawaida au kurudia nyimbo za zamani.

Leo, Alikiba ameachia wimbo wake aliyouita mpya wa ‘HELA’ ambao kiukweli sio mpya ni wimbo wa miaka mitatu iliyopita na hata kipindi hicho haukuwa mkali kivile, sasa kwanini unakuja kuurudia mwaka 2018?

Sitaki kuamini kama Alikiba ni mvivu kiasi hicho au ameridhika kiasi kwamba anashindwa kuumiza kichwa na kutunga nyimbo kali kama alivyozoeleka.

Leo mapema baada ya kuachia wimbo huo, hayakupita hata masaa matatu Alikiba alishambuliwa sana na mashabiki wake wengi wakimwambia aache kurudia nyimbo, wengine wakishindwa kuamini kama ni yeye aliyefanya maamuzi ya kuachia video ya wimbo huo. Pitia baadhi ya maoni ya wadau mitandao baada ya kuachia wimbo wa HELA

officialkisimpleKiukweli umetukosea sana mashabiki wako na unavyoelekea utapotea kimziki tuambie moja km unataka kuacha mziki bora uache tujue moja maana cc ndio tunaopata tabu bro yaan umetuferisha 😂😂mashabiki zako wanakimbia bro

raquiz_star_boyWe jamaa m shabiki ako namba moja ila hi nyimbo kaka umezingua nenda na wakat bn hela ndio nn kaka man piga nyimbo za kuchezeka clb hzo nyimbo za kuimba bungen hela hela hela

nyangephotoHuwa sikomenti hata kama unakosea. Nakukubali sana. Ushahuri tu bro, hizo nyimbo za zamani zilikua na ni nzuri. Kuzirudia kwa sasa kama project za kibiashara nadhani hahitakusaidia kitu bro. Mashabiki wengi wanafikiri kama mimi.

Honestly, nadhani King Kiba is overrated. Ana kipaji cha hali ya juu lakini sijui tatizo ni management au uzembe wake mwenyewe. Labda aelekeze nguvu zaidi kwenye soka (naongea haya kama Team Kiba).
emmanuelraisKing umeyumba mzee wakati|mda huu hukutakiwa kutoa ngoma ambyo tayari audio ilishasikilizwaga kitambo, Ila sema nini 2naishinao.
mpasukooJamani mimi team mond lakin kusema ule ukweli @advocate.fi alikiba anazingua sana analeta mazoea na mziki.
pambakyotoWe jamaa sio mzima kwa kweli watu tumekaa mkao wa kula tunasubiri chakula tule umetulisha mavi SAA hivi tunatapika tu badilika brother unachosha sio siri hivi unApata wapi ujasiri wa kujiita king kwa haya madudu unayoyatoa sasa hivi kuliko kuendelea kutudhalilisha mashabiki wako mitaani basi nikushauri staafu mziki kwa heshima ili uendelee kucheza mpira mana sio kwa maboko haya

Alikiba hakuchukua hata masaa manne akaifuta video ya wimbo huo, na mpaka sasa hajazungumzia chochote kuhusu kufutwa kwa video hiyo.

Mimi naamini Alikiba unauwezo mkubwa kwenye muziki, watendee haki mashabiki wako kwani hao ndio wanaoumia zaidi na bila wao wewe si kitu.

Kwa mwaka huu sitaki kuamini kuwa kitendo cha kujiingiza kwenye soka kimepelekea ushuke kimuziki HAPANA. Naamini umebweteka kwa vile unajua una uwezo ukubwa bila kukumbuka kuna msemo usemao “HARDWORK BEATS TALENT”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents