Burudani ya Michezo Live

Makala: Msanii kuachia wimbo exclusively kwenye radio moja kwanza kunavikera/udhi vituo vingine

Chukua mfano, una rafiki yako ambaye ana rafiki mwingine pia. Ananunua icecream ambayo anampelekea kwanza rafiki yake mwingine anayeila kisha kuibakiza, halafu rafiki yako anakuletea uimalizie wewe. Maana yake ni kwamba anakuletea makombo, utafurahi? Sio rahisi ukafurahi.

14311372-grunge-rubber-stamp-with-the-word-exclusive-written-inside-the-stamp

Kwa mfano huo hebu twende kwenye mada inayohusika. Hivi karibuni kumepamba moto mtindo wa wasanii kwenda kuachia nyimbo zao mpya exclusively kwenye vituo kadhaa vya radio. Mara nyingi vituo vinavyopata bahati hiyo ni Clouds FM na East Africa Radio, labda kwa sababu ya umaarufu wa vituo hivyo. Vituo vingine vya radio husubiri kutumiwa nyimbo hizo baada ya kuchezwa exclusively kwenye radio hizo.

Si jambo geni hata hivyo. Vituo vya runinga kama BET na MTV huwa na kitu kama hicho pia. Lakini kwa Tanzania, uamuzi huu una faida ama una hasara zaidi? Kama usemavyo mfano hapo juu, ni wazi huu ni uamuzi ambao watangazaji wa radio zingine huutafsiri kama dharau. Kitendo hicho kinatafsiriwa na mtangazaji wa kipindi cha African Beats cha Kiss FM, Dee Seven kama matusi.

“Hi ni kwa wasanii wote mnaotoa kazi zenu na kuzifanya exclusive kwa radio fulani kisha baada ya wiki ndo mnasambaza radio nyingine plzzz naomba msinitumie kabisaa song hizo coz ni usen¥*..,track inatambulishwa na kuchezwa kwa hiyo wiki then inatupwa kapuni halafu ndo mnaanza kutusumbua blaza…blaza nakutumia ngoma yangu mpya…fu¥*k that shit… #THE-UGLY-TRUTH,” ameandika Dee Seven kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwa mfano wa icecream hapo juu, kama rafiki yako akikuletea icecream iliyoliwa kwanza na rafiki yake mwingine, lazima utahisi amekudharau na kwamba anamthamini zaidi rakifi yake mwingine. Wewe utajihisi kama chaguo la pili baada ya huyo mshkaji wake mwingine. Watangazaji na madj wa radio zingine huzipokea nyimbo zinazozinduliwa kwa mtindo huu kwa shingo upande. Ndio hivyo, wengine huchukia na kukataa kuzicheza kabisa. Nyimbo za kucheza zipo nyingi, hivyo dj kama huyo haoni hasara kuiweka kapuni ngoma yako, si umemdharau bwana!! Kwanini sasa ajipendekeze?

Kama unataka kuachia wimbo kwa dizaini hii, basi hakikisha kuwa ni mkali ili hata kama watangazaji wengine wakichukia, hawana jinsi ya kufanya uwatumiapo, lazima waucheze kwasababu ni hit. Kama ni ya kawaida ama tuseme ni mbovu, madhara yake ni makubwa zaidi.

Ili msanii uwe kwenye ‘safe side’ ni bora kila kituo ukakipa haki ya exclusivity. Hii ni kwasababu kila msikilizaji ana radio yake anayopenda kusikiliza. Wakumbuke wasikilizaji hao pia kwa kuwafanya wa kwanza. Kwasababu kuna maeneo mengu radio hizi zinazopewa exclusivity hazisikiki. Onesha kuthamini kila kituo cha radio kwa kuzipa priority sawa, sio dhambi kufanya hivyo.

Kazi kwako msanii, kusuka ama kunyoa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW