Makala: Nandy umetudanganya, umezidi kumpa ushindi Zari (+Audio)

Kwanza nitoe pole kwa Nandy na Bill Nass mara baada ya video yao ya faragha kuvuja mtandaoni, ni kitu ambacho unaweza kukichukulia kawaida ila usiombe yakukute.

Viatu walivyovaa Nandy na Bill Nass kwa sasa vinawapwaya katika miguu yao na pengine ni vizito, nitoe pole kwao kwa hilo lilowafika kwani ni tukio ambalo si vigumu kuja kufutika katika maisha yao kutokana na utandawazi uliopo sasa.

Fid Q katika ngoma yake August 13 alisema, ustaa ni mzigo wa mwiba, ukiubeba utaumia. Video ya Nandy na Bill Nass imesambaa kwa kasi kutokana na umaarufu wao, hivyo maumivu wanayopitia wanapaswa kuelewa ni kawaida katika tasnia yao ya burudani.

Nandy ameelewa hilo na ndio sababu hakuona aibu kuomba radhi kwa mashabiki wake kwa hicho kilichotokea. Kwa anayeelewa maana ya neno samahani atakuwa amemsamehe na maisha mengine kuendelea.

Kwanini Nandy

Baada ya video kusambaa, Nandy na Bill Nass kila mmoja amejitetea kwa upande wake. Nimzungumzie Nandy kwa ufupi; ameomba radhi na kueleza kilichotokea ila kuna jambo halipo sawa kwa upande wake.

Kwa mujibu wa post aliyoweka Bill Nass katika ukurasa wake wa Instagram jana na kuifuta baada ya muda mfupi alitupa lawama zake nyingi kwa Nandy kuhusu kuvuja kwa video hiyo. Ameeleza siku moja kabla, Nandy alimtafuta kumuomba picha za zamani kipindi wakiwa wapenzi ili azitumie katika kum-wish Happy Birth Day yake, hata hivyo alimueleza kuwa hana picha hizo.

Lakini baadaye alikuja kuona picha hizo mtandaoni kitu ambacho hakupendezwa nacho kutokana kwa sasa ana mahusiano mapya, hivyo Nandy alishindwa kuheshimu uamuzi wa mwenzake.

Katika Interview aliyofanya Nandy na MCL Digital alieleza kuwa walikuwa na mahusiano mwaka 2016, mahusiano yao walipanga kuwa private lakini ukifuatilia kwa makini kuna kitu ambacho hakipo sawa hapa.

Katika video iliyosambaa mtandaoni unasikika wimbo wa Bill Nass unaokwenda kwa jina la Sina Jambo. Wimbo huu ulitoka Augost 17, 2017, yaani miezi saba iliyopita.

Hivyo kueleza kuwa walikuwa na mahusiano mwaka 2016 na ndio video hiyo ilirekodiwa, bado haiingii hakilini kwa urahisi huo.

Kuhusu Zari

Sikupenda kumhusisha mrembo huyo katika suala hili ila kutokana na ujumbe ambao ningependa kuutoa nalazimika kufanya hivyo. Nitangulize samahani kwa yeyote nitakayemkwanza.

March 28, 2018 mwaka huu Zari alipata dila la kuwa balozi wa kutangaza nepi za watoto za Soft Care. Baada ya hapo kulizuka mjadala kuwa ni kwanini mastaa wa kike Bongo hawajapewa dili hilo au kupata dili kama hizo.

Muigizaji Faiza Ally alihoji; ” how stupid Tanzanian can be, mastaa wote watanzania, watu wote Watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya Zari ? Ina maana uhitaji Bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje?.

Baada ya kauli hiyo Shamsa Ford alimjibu Faiza kwa kumueleza kuwa hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua staa wa Bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara.

Aliongeza kuwa baadhi ya mastaa wengi wa Bongo wanajulikana kwa mambo ambayo si mazuri kitu ambacho si kizuri kwa brand za kibiashara.

“Maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika.kikubwa tujifunze, swala sio kujulikana ila swala ni kuwa unajulikana vipi!? Watu wanakutambua kwa lipi. Ni vizuri tumeumia sasa tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika,” alisema Shamsa.

Kwa mujibu wa posti ya Bill Nass, alieleza baada ya kumuuliza Nandy ni kwanini ametoa picha hizo za kitambo wakiwa katika mahusiano kwani ni kitu walipanga kuwa siri, Nandy alimjibiwa kuwa amepanga kiki yeye na team yake. Weka nukta hapo.

Twende pole pole; Kwa kile kilichotokea jana kwa Nandy naanza kuelewa kile alichoeleeza Shamsa Ford. Sielezi kwa kumhukumu Nandy, hapana!, ila ni ukweli ambao upo na utendelea kuishi. Hivyo maneno ya Shamsa yanasaidifu kile kilichotokea kwa asilimia kubwa na tukio lenyewe linatoa sababu ya kwanini Zari alistahili kupata dili lile. Asante.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW