Bongo5 Makala

Makala: Nay, Quick Rocka na Saida Karoli, wametaka ganda la ndizi au ubunifu hawana?

Mwezi huu wenye siku 30 umekuwa wenye simulizi nyingi za burudani na michezo. Kiufupi ni mwezi wenye historia yake kama umeufuatilia kwa makini.

Mwezi huu tumeshuhudia nchi ya Tanzania ikitembelewa na wachezaji wa mpira akiwemo mchezaji wa zamani wa Uingereza na klabu za Manchester United, David Beckham, beki wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya Ufaransa, Schneiderlin pamoja na mchezaji wa Tottenham, Victor Wanyama.

Kwa upande wa burudani tumeshuhudia mengi, kwa mfano uzinduzi wa filamu mpya ya Gabo ‘Kisogo’ aliyomshirikisha Wema Sepetu, filamu hii itaonekana kupitia app, huu ni mwanzo wa mapinduzi katika namna ya kuuza kazi za sanaa kuendana na wakati.

Hapo hapo kwenye buruduni, kwa upande wangu nimekuwa busy sana katika kusikiliza ngoma tatu tu!, ambazo zimetoka mwezi huu. Yakwanza ni Orugambo ya Saida Karoli, Moto ya Nay wa Mitego, na ya tatu ‘Watasema’ ya Quick Rocka na OMG ambayo imetoka jana.

Kwanini Saida Karoli, Nay wa Mitego na OMG

Katika nyimbo hizo tatu nilizotangulia kuzitaja, kama ubahatika kuzisikiliza bila shaka utagundua zimechukua maneno, beat au melody kutoka kwenye wimbo au nyimbo fulani. Kumbuka zote zimetoka mwezi huu (June) wenye siku 30 na masaa 720.

Katika wimbo wa Saida Karoli ‘Orugambo’ ambao video yake ilitoka June 12 mwaka huu, amechukua baadhi ya maneno kutoka kwenye nyimbo tatu tofauti. Amechukua kutoka kwenye wimbo wa Diamond ‘Salome’, amechukua kwa Belle 9 ‘Give It To Me’, na mwisho kutoka kwa Darassa katika ngoma ya Muziki.

Kwa upande wa Nay wa Mitego katika ngoma yake ya Moto, amechukua maneno na malody kutoka kwenye nyimbo tatu, amechukua kutoka kwa Balozi ‘Kwenye Chati, pia amechukua kwa Juma Nature ‘Hili Game’ pamoja na ngoma ya Mchizi Mox ‘Mambo Vipi’. Mapokeo yangu ngoma hii ni makubwa kwa upande wa mashabiki wa Nay ambao hupenda yeye anavyowachana watu wazi wazi, tuachane na hilo.

https://youtu.be/t19V0W0-Y-g

Tukiangalia ngoma ya OMG ‘Watasema’ ambayo wamemshirikisha Quick Rocka ambaye ni kama boss wao, ngoma yao imechukua chorus kutoka kwenye wimbo wa TID a.k.a Mzee Kigogo ‘Watasema Sana’ iliyotoka zaidi ya miaka 10 nyuma. Well done, wote wamenifurahisha kwa ngoma zao.

Hoja yangu

Binafsi nimekuwa nikijiuliza nini maana ya mfululizo wa nyimbo za aina, naomba nisinukuliwe vibaya, sijapiga, ila nyimbo za aina hii zinatoa picha ya aina gani katika muziki wetu?. Muziki umekua, wasanii wanatafuta uwepesi au wasanii wameishiwa ubunifu. Yote yanaweza kuwa majibu.

Saida Karoli ni msanii wa siku nyingi na ukubwa wa jina lake unaheshimika zaidi miaka 15 sasa, kuchukua baadhi ya vitu kutoka kwenye nyimbo za Belle 9, Diamond na Darassa ambao pia walichukua nao kutoa kwenye wimbo wake wa Maria Salome ni sawa kwa sababu anatafuta kujenga ushiwishi kwa wanunuzi wa bidhaa yake kwa sasa ambao wengi ni vijana.

Ni wazi wimbo huu umependwa kutokana na nyimbo hizo tatu kufanya vizuri, hivyo Saida Karoli amepata wepesi katika mapokeo ya wimbo huo. Je huu uwepesi ulikuwa akiutafuta au umekuja kwa bahati mbaya?, ni vigumu kusadiki hilo kwa sasa, hivyo naomba tuachane nalo.

Nay wa Mitego na ngoma za Mchizi Mox, Balozi na Juma Nature, je anatafuta ushawishi katika kizazi cha sasa au kilichomtangulia (old school)?, kama ni sasa mbona Nay anafahamika na kazi nyingi ambazo hadi zinapendwa na viongozi wakubwa serikalini, kama ni kwa upande wa old school njia aliyotumia nina mashaka nayo. Kizazi hicho hakiwezi kumkubali kwa kurudia kile ambacho wameshakifanya, hivyo hapa Mr Nay angetakiwa kuwa mbunifu kwa kuleta kitu kipya ambacho kingekuwa na nguvu ya ushawishi kwa pande zote mbili.

OMG ni miongoni mwa makundi machache yanayofanya vizuri kwa sasa katika muziki wa hip hop Bongo, wanaonekana watafika mbali. Binafsi sikuona sababu ya wao kuchukua chorus ya TID kwa namna walivyofanya vizuri na wimbo wao ‘Uongo Na Umbeya’, katika wimbo wao verse ya kila mmoja ni kali, kwenye flow kama kawaida yao huwajawahi kuniangusha, ila chorus!!!.

Quick Rocka ameitendea haki chorus, ameonyesha uwezo wake wote na kweli kitu kimetoka kikali sana, ila kulikuwa na ulazima gani kuchukua chorus ya wimbo mwingine. Sitaki kuamini OMG na Quick Rocka walishindwa kuandika chorus, pengine hawakutaka kuwa wabunifu zaidi kwenye hili, walichukulia poa, walizembea, yote pia yaweza kuwa majibu, ila niwapongeze kwa kazi nzuri waliyofanya.

Bado kuna tatizo

Kurudia au kuchukua mashairi, beat au melody katika wimbo mmoja au zaidi na kwenda kutengeneza mwingine si kitu kibaya, ni jambo ambalo lipo duniani kote ila kwa namna tunavyolifanya hapa Bongo napata wasiwasi, pengine labda ya ugeni wa jambo hilo.

Saida Karoli alipoulizwa kwa nini ameamua kutumia vya Diamond, Belle 9 na Darassa, alijibu amefanya hivyo kwa kuwa nao walichukua vya kwake

“Walitumia vionjo vya wimbo wangu wakijua mimi nipo hai ndio maana na mimi nikachukua vyao kama walivyochukua vyangu, nikatengeneza muziki na namshukuru Mungu umepokelewa vizuri sana,” alisema Saida.

Katika huku na kule kuna tetesi kuwa hakuna aliyemlipa katika ya hao watatu, pia kuna mmoja wapo hata hajawahi kuongea na Saida, hivyo kuna uwezekano mkubwa mambo hayo yanapelekwa kienyeji tu.

Hiyo jana masaa kadhaa mara baada ya OMG kuachia video ya wimbo wao ‘Watasema’ TID alikuja juu kama moto wa kifuu, watoto wa mjini wanasema ametokwa povu, na kudai atawashtaki OMG na Quick Rocka kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake.

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema, ameandia msanii huyo. Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.”

Hiyo hapo juu ni post ya TID katika mtandao wa instagram. Binafsi naunga mkono wasanii kuazimana vionjo katika nyimbo zao ila basi kuwe na makubaliano yatakayonuisha pande zote mbili. Ila huku ni muziki kukua, wasanii wanataka wepesi au wasanii hawataki kuwa wabunifu?. Naomba kuwasilisha.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents