Michezo

Makala: Unaifahamu El Clasico na umuhimu wa kushinda kwake ?, hii ndiyo historia ya mtanange huu uliyojaa ubabe

Hapo kesho siku ya Jumapili majira ya saa 12 za jioni dunia itanyamaza kwa muda kupisha mtanange mkubwa na wa haina yake ambao utaangaziwa na robo tatu ya mashabiki wa soka ulimwengu kote hasa kutokana na uzito wa mechi hiyo hiyo baina ya miamba miwili ya soka kutoka nchini Hispania mabingwa wa La Liga klabu ya Barcelona dhidi ya mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya timu ya Real Madrid.

Ukubwa wa mtanange huo hasa unatokana na uhusiano wa timu hizo toka miaka ya 1902 wakati klabu hizo zilipokutana kwa heshima ya mfalme Alfonso XIII. Uhasama ukaongezwa nguvu zaidi pale ambapo utawala wa Fransinco Franco Bahamonde aliyetaka kuififsha Identity ya Barcelona na Kuipendelea zaidi Real Madrid.

Siasa zilichagiza zaidi uhasama wa miamba hii miwili ya soka nchini Hispania wakati jimbo la Catalonia Linatambulishwa zaidi na itikadi pamoja na tamaduni zinazojitegemea ambazo zinatofautiana na upande wa serikali kuu. Na wakazi wa Catalonia wanaelezea kuwa jimbo lao lilokuwa huru kabla ya kuanguka kwa dola ya utawala uliotawala Hispania na Ureno.

Kutengwa kwao kwa muda mrefu wakazi wa jimbo la Catalonia walinyimwa nguvu za kisiasa na kuanza kutumia klabu ya Barcelona kama ni sehemu ya kuonesha hisia zao na katika uongozi wa Franco Klabu ya Barcelona ikatambulisha utambulisho na uhalali wa jimbo lao kama ni nchi tegemezi na wanapinga uvamizi wa Serikali kuu ya Madrid.

Ukiangalia Nembo ya Fc Barcelona Inaandikwa “Mes Que Un Club” kwa lugha ya Kispanyola lakini kwa Tafsiro ya kiswahili ni kusema “Hii Ni Zaidi Ya Klabu”. Tukirudi Katika El classico hii Itawakosa wachezaji Nyota Messi na Cr7 ambapo Messi ameumia sehemu ya nyama za bega na Upande wa Ronaldo amehama Madrid na kwenda kuitumikia Juventus Turin.Wachezaji hawa kiujumla ndio Icon ya mpira wa Dunia kwa Takribani miaka 10 sasa huku wakiwa kwenye Ubora wa hali ya juu mno.

Image result for el clasico

Madrid katika michezo mitano iliyopita  kwenye mashindano yote wamepoteza mechi 3, sare mechi 1 na ushindi mechi moja wakati Barca wameshinda mechi 3 na Sare mechi 2.

Barcelona Wataingia na Historia ya kufunga Goli katika kila mchezo waliocheza Dhidi ya Real Madrid kwa jumla ya michezo 21 ya mwisho Na Kwa upande wa Real Madrid walifanya hivyo mwaka 1959 mpaka 1969 kwa jumla ya michezo 22 mfululizo.

Image result for el clasico

Rekodi zinaonyesha Real Madrid wataingia wakiwa hawajafungwa katika michezo minne waliocheza katika uwanja wa Camp nou ambapo wameshinda mchezo mmoja na Sare michezo 2. Wakati Barcelona wanaingia na rekodi bora ya kutofungwa katika uwanja wa Camp Nou kwa takribani mechi 41 za ligi ambapo wameshinda michezo 33 na sare michezo 4.

Image result for el clasico red card

Baadhi ya majeruhi washaanza kurejea katika hali ya kawaida akiwemo Beki wa Pembeni wa Real Madrid Marcelo. Makocha wa pande zote mbili wameongelea kuhusu mchezo huku inatambulika kuwa kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui ana wakati mgumu sana wa kuweka kubaki kutokana na matokeo mabovu na mwanzo mbaya kwa Real Madrid na Kufikiria Kumchukua kocha mwengine baada ya mechi hii.

Image result for el clasico

Wachambuzi wa soka wameonesha Kuishusha hadhi Real Madrid baada ya kuondokewa na kocha Zinedine Zidane pamoja na Cristiano Ronaldo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents