Bongo5 Makala

Makala: Vijana tuyaonee wivu maisha ya JK baada kustaafu

Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete aliyeingoza Tanzania kuanzia mwaka 2005 hadi 2015, tangu kustaafu kwake ameamua kujikita zaidi katika kilimo kitu ambacho ingekuwa ni vigumu kutabiri kama angefanya hivyo kabla ya kustaafu kwake. Kilimo ambacho vijana wengi tunakichukulia poa, sasa ngoja nikueleze jambo.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012 nchini ilibainisha idadi ya Watanzania ni milioni 44,929,002, na ilikadiriwa ifikapo mwaka 2016 idadai hiyo itaongezeka na kufika milioni 51,000,000 na kulingana na Sensa hiyo asilimia 34.7 ya watu wote nchini ni vijana wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35.

Kilimo nilichotangulia kukitaja inakadiriwa kuajari zaidi ya asilimia 70 ya watu nchini ambapo kwa mwaka 2015 kilichangia karibu asilimia 50 ya pato la taifa na asilimia 7 ya biashara za nje. Lakini bado idadi ya watu wanaojighusisha na kilimo inazidi kupungua hasa vijana, wengi tumekua tukiamini katika kazi za kuajiriwa hasa za mijini na ndio sababu kila uchwao idadi ya watu inazidi kuongezeka mijini ingawa si kitu kibaya.

Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete akiwa shambani

Takwimu zinaonyesha asilimia ya watu wanaoishi mijini imeongezeka zaidi ya mara tano ambapo ni asilimia 6.4 mwaka 1967 na kufikia asilimia 29.6 kwa mwaka 2012.  Hii maana yake nini?, ni kwamba kuna uwezekano mkubwa idadi ya wanaojighusisha na kilimo kupungua kwani nguvu kazi kubwa ina hama kuja mjini bila kujua kwenye kilimo kuna fursa pia.

Kilimo Kinalipa

Mwaka 2015 katika Kipindi cha Mkasi, Mtanzania Mohammed Dewj (MO) ambaye mwaka huu ametajwa na jarida la Forbes kama bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.4 bilioni, alisema vijana wanaotamani kuwa kama yeye ni lazima waingie katika kilimo.

Mohammed Dewj (MO)

Mohammed Dewji (MO) ambaye wiki iliyopita alifanikiwa kukutana na tajiri namba moja duniani na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates, katika tv show hiyo alijaribu kueleza namna ukuaji wa uchumi nchini, Afrika na dunia utavyoweza kumgusa mwananchi wa chini na kuonya kuwa hilo halitofanikiwa kama hawatojighusiha na kilimo.

“Nchi yetu ni top ten fast growth economy in the world, uchumi wa dunia unakua kwa asilimia 1.8 kwa wastani, Afrika uchumi wake unakua kwa asilimia 5 lakini Tanzania uchumi wetu unakua kwa asilimia 7. Tatizo hiyo pesa haiwafikii watu chini, ni lazima tujipange tutoke kwenye asilimia 7 mpaka asilimia 12 hapo ndipo watu wa chini wataona pesa.

“Ni lazima tuwekeze nguvu kubwa kwenye kilimo na vijana wengi hawataki kulima sasa kuna ongezeko kubwa la watu mjini. Lakini niwaambie siri moja vijana wenzangu, mimi nipo kwenye kilimo cha katani, chai, korosho na ninatengeneza hela nyingi,” alisema Mohammed Dewji (MO).

Rais Mh. Mstaafu Kikwete katika moja ya picha zake akiwa shambani aliandika, “Kuna maisha baada ya Urais hususani wasaa wa kufanya yale uliyokosa muda wa kuyafanya kama kutumia muda na familia, kuangalia mifugo na shamba,”.

Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete

Vijana walio katika ajira rasmi ni vema wakafikiria namna ya kuwekeza katika kilimo ili kuwa msaada wao pindi watakapokuwa nje ya ajira zao kwani ushindani wa ajira kwa sasa ni mkubwa. Utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wa mwaka 2014 unaonyesha watu 2,141,351 sawa na asilimia 4.3 ya wa Tanzania bara ndio walioajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi ambayo ameajiri asilimia 67 ya wote wenye ajira nchini, je hao wanaobaki wapi wanaenda?, hapo ndipo unakuja umuhimu wa kujighusisha na kilimo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents