Bongo5 Makala

Makala: Wanasiasa mnaohama vyama mnawaweka njia panda wapiga kura wenu (+video)

Hivi karibuni kumekuwa na Wanasiasa wengi ambao wamekuwa wakitoka chama hichi kwenda kingine kwa kutoa sababu zao tofauti tofauti na binafsi.

Wapo sahihi kutokana wametumia haki yao ya Kidemokasia lakini maamuzi yamefanyika kwa wakati ambao wananchi waliowachagua walikuwa bado wanawategemea katika kuleta maendeleo. Wananchi hao wanakuwa njia panda kushindwa kushindwa kuelewa waamini lipi kati ya ahadi wanazozitoa majukwaani.

Mnamo Novemba 30 aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alitoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuacha nafasi ya Ubunge wa Jimbo lake na kujivua uanachama kuelekea Chama cha Demokrasia na Manendeleo Chadema kwa kutoa sababu zifuatazo:

“NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM.”

Novemba 21, Aliyekuwa Waziri wa Mambo wa Ndani na mwanachama wa CHADEMA, Lawrence Masha ameomba kupokelewa katika chama chake cha zamani cha CCM alichokihama wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka 2015. Lawrence Masha nae alijiunga a Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vikao vya Chama hicho vinavyoendelea Ikulu jijini Dar es salaam na kusema kuwa ”Nimekuja hapa kuwaombeni mnipokee mwana mpotevu nimerudi, Niko imara na nitakuwa mwaminifu kwa CCM.”

Siku ambayo Lawrance Masha ndio siku ambayo aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa Chadema, Potrabas Katambi alikihama chadema na kuhamia CCM siku ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi huku akidi kuwa hajalazimishwa na mtu na wala wazazi wake hawakujua kama atahamia katika Chama hicho. Patrobas alesema “Nilichokiona huku muheshimiwa Mwenyekiti ni kwamba kama leo nikuita msaliti nasaliti ubinafsi na kundi la wabinafsi kwa maslahi ya taifa , maisha tunayoyaishi majukwaani sio maisha ambayo tunayo unaweza sema tuna maendeleo unaweza kwenda jimboni kwa mtu ukakuta hakuna maendeleo anayoyasema.

Naye, Wakili Msomi aliyewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando amejiunga na Chama Cha Mapinduzi katika vikao kilichofanyika Ikulu siku ie ile na kueleza kuwa “Chama cha Mapinduzi kiliahidi ajira tunaona juhudi zinazofanyika na serikali kutengeneza ajira , chama cha Mapinduzi kiliahidi kupambana na ufisadi na rushwa sasa hivi tunaona ni watu wa aina gani wana chuchumaa Mahakamani ni watu wa aina gani wanapandishwa kwenye karandinga,” alisema Msando.

Oktoba 19, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa wa Chama Cha ACT Wazalendo, Samson Mwigamba alitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kujiuzulu uongozi wa chama hicho. Kwa kile alichokieleza kwa waandishi wa habari kuwa anaunga mkono Chama cha Mapinduzi lakini jambo jingine alisema kuwa ameona kwasasa ufisadi una enda vyama vya upinzani.

Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia CUF, Maulid Said Abdallah Mtulia alikihama Chama hicho na kuhamia rasmi Chama cha Mapinduzi ambapo alikabidhiwa rasmi kadi ya chama na kupokelewa kwa shangwe katika ofisi za chama hicho Kinondoni, Dar es salaam.Ambapo alieleza sababu kuwa amekihama Chama hicho kwa kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Naye Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ambaye baada ya kushindwa ubunge mwaka 2015 alihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka jana na siku kadhaa zilizopita amehamia Chama cha Mapinduzi CCM. Mzunguko wa Kafulila kuhama vyama upo hivi alitoka (NCCR-Mageuzi kwenda Chadema na baada ya hapo kahamia CCM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents