BurudaniMakala

Makala: Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan

Diamond Platnumz wiki hii amemkubali mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto atwaye Abdul aka Dylan kuwa ni mwanae baada ya kumkataa mtoto huyo kwa lengo la kumficha mama watoto wake, Zari The Bosslady ambaye tayari amezaa naye watoto wawili, Princes Tiffah pamoja na Nilan.

Hamissa Mobetto akiwa na baba Diamond kwenye arobaini ya Dylan iliyofanyika siku chache zilizopita

Rais huyo wa WCB amedai alikubaliana na mwanamitindo huyo kulifanya jambo hilo kuwa siri ili kulinda heshima yake na familia kwa ujumla kitu ambacho hakikufanikiwa.

Bongo5 imeamua kurudi nyuma na kuangalia ni siku gani na wapi Diamond na Hamisa Mobetto walikutana na kufanya mchakato wa kupatikana kwa Dylan ikiwa mtoto huyo alizaliwa 8/ 8/ 2017 katika hospitali moja hapa jijini Dar es salaam.

Wataalamu wa afya wanasema mwanamke hujifungua mtoto baada ya miezi tisa toka siku ambayo mimba imeingia. Pia kuna baadhi ya wanawake hujifungua kabla ya siku hizo kutokana na matatizo ya kiafya ambapo mtoto anayezaliwa kipindi hicho uitwa njiti na huwa katika uangalizi maalumu.

Lakini mtoto wa Mobetto, Dylan amezaliwa kawaida kulingana na taarifa ambazo aliziweka wazi mwanamitindo huyo na kama ni hivyo basi wawili hao walivunja amri ya sita mwezi Novemba mwishoni mwaka 2016 au Disemba mwanzoni. Je swali lilipo ni wakati gani na wapi wawili hao walikutana, hebu tungalie matukio ambayo yalitokea mwezi Novemba na Disemba ambayo bila shaka yalikuwakutanisha wawili hao wakati Zari akikaribia kujifungua mtoto, Nilan, Disemba 6 2016.

Salome yawakutanisha.

Video ya wimbo ‘Salome’ ndio project ya kwanza kuwakutanisha wawili hao baada ya mwanamitindo huyo kucheza vitendo katika video ya wimbo huo.

Licha project hiyo kuwaweka karibu zaidi wawili hao lakini mapaparazi waliufuatilia ukaribu wao na kugundua kuna kitu kinaendelea kati yao huku mashabiki wakibaki na kumbukumbu ya neno ‘project’ ambalo pia liliwakutanisha kimapenzi Diamond na Zari.

“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm.

Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”

Naye mwanamitindo huyo alivunja ukimya baada ya kuona stori za mahusiano yao zinachukua sura mpya hasa hasa baada kuona picha zake zinasambaa mtandaoni akiwa chumba kinachofanana au alichowahi kukitumia zari na Diamond wakiwa Afrika Kusini.

“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.

“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza tumekutana ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza. “Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.” alisema Mobetto.


AFRIMA: Diamond na Mobetto watua Lagos Nigeria.

Novemba 6 mwaka 2016 zilifanyika tuzo za All Africa Music Awards, AFRIMA, Lagos Nigeria. Usiku wa tuzo hizo uliwakutanisha mastaa mbalimbali wa muziki wa mataifa akiwemo Diamond ambaye ali-perform usiku huo.

https://www.instagram.com/p/BMcJt8djA2R/?taken-by=diamondplatnumz

Katika usiku huo wa tuzo Diamond Platnumz aliibuka na ushindi wa nguvu wa tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa.

Tetesi zinadai muimbaji huyo alisafiri nchini humo na mwanamitindo, Hamisa Mobetto hivyo basi baada ya ushindi huo bila shaka muimbaji huyo alipokea mabusu moto moto kutoka kwa mwanamitindo huyo mwenye umbo na muonekano wa kuvutia.

“Wakati tunarudi Lagos tulikuwa na Hamisa Mobetto, Diamond alikuwa VIP na sisi tulikaa business class,” alisema mmoja kati ya watu wa crew yake akiweka sharti la kutokutajwa jina lake.

Hata hivyo mwanamitindo huyo hakuwa anapost chochote kuhusiana na tukio hilo huku wadau wa mambo wakidai huo ulikuwa ni mpango maalumu wa kulifanya jambo hilo kuwa siri.

Diamond atua Full Moon Party, Mayotte na Zimbabwe

Muimbaji huyo baada ya kurejea nchini Tanzania siku sita baadaye, Novemba 12 aliibukia kwenye show ya Full Moon Party iliyofanyika Kendwa Rocks, Zanzibar. Show hiyo ilikuwa ya aina yake kutokana na kuwakusanya watu kutoka mataifa tofauti tofauti. Hata hivyo haikujulikana kama pia show hiyo alisafiri na mwanamitindo huyo.

https://www.instagram.com/p/BMyglDjjPAi/?taken-by=diamondplatnumz

Novemba 24 Diamond alitua Mayotte nchini Ufaransa, ambapo alipokelewa kwa shangwe na watanzania ambao walijitokeza kwa wingi katika uwanja wa ndege wa mji huo. Muimbaji huyo alifanya show mbili ambapo moja ilikuwa ya kawaida na nyingine ilikuwa ya VIP.

Baada ya show hizo muimbaji huyo alielekea nchini Zimbabwe ambapo alifanya shows zaidi ya tatu na Disemba 5 2016 alisafiri na mama yake kwenda nchini Afrika Kusini sehemu ambayo Zari alikuwa anajifungua mtoto wake wa pili.

Tetesi za mimba ya Mobetto zaanza kuzagaa kwa kasi.

Ingawa kulikuwa na usiri mkubwa lakini mambo yalianza kubadilika kwa Mobetto, Juni 21 2017 tetesi za mwanamitindo huyo kuwa ana mimba ya Diamond zilizagaa kwa kasi.

Hata hivyo Diamond akihojiwa na kipindi cha Leo Tena Cha Clouds FM alikanusha kumpachika mimba mrembo huyo.

“Toka nimeshoot video na Hamisa Mobeto wimbo wa Salome, watu wamekua wakituhusisha pamoja, ujauzito wa Hamisa sio wangu. Jamani mwenye mimba si ajitokeze, si unajua hata mtu wake atakuwa anajisikia vibaya,” alisema rais huyo wa WCB.

Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan

Zari the Boss Lady alijifungua Dylan Disemba 6 mwaka 2016, naye Hamisa Mobetto amejifungua 8/8/2017 kwa maana hiyo kama mwanamitindo huyo alijifungua baada ya kutimiza miezi 9, basi Diamond na Mobetto walikutana na kuvunja amri ya sita mwezi Octoba ama Novemba wakati Zari ana siku chache za kwenda kujifungua.

https://www.instagram.com/p/BNrHM9XjgUv/?taken-by=diamondplatnumz

Novemba 6 mwaka 2016 zilifanyika tuzo za All Africa Music Awards, AFRIMA, Lagos Nigeria ambapo muimbaji huyo alidaiwa kusafiri na Mobetto na kutoka na mahesabu haya huwenda Diamond na Mobetto walivunja amri ya sita Nigeria na kufanikisha kupatikana kwa mtoto Dylan. Je ni kweli wawili hao walikutana Lagos hebu na wewe jaribu kuchanganua na utoe maoni yako kwani kipindi hicho chote Zari alikuwa akijitazamia kujifungua nchini Afrika Kusini hivyo isingekuwa vizuri kwake kuzunguka pamoja na Diamond katika show zake mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents