Michezo

Makampuni yajipanga mstari kutaka kumdhamini Pacquiao baada ya Nike kumtosa

Mchezaji masumbwi wa Ufilipino, Manny Pacquiao anafanya mazungumzo na makampuni ya bidhaa za michezo baada ya Nike kusitisha mkataba naye kufuatia kauli yake kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

Pacquiao-breaks-camp_120604_006a

Nike ilivunja udhamini wake kwa bingwa huyo wa mara nane wa dunia baada ya kuwaelezea mashoga kuwa ni wabaya zaidi ya wanyama. Kauli yake hiyo iliwakasilishwa watu wengi hususan wale wanaojihusisha bna mapenzi ya aina hiyo.

Meneja wake Eric Pineda ameliambia shirika la habari la AFP kuwa makampuni mengi yanataka kumpa udhamini. Amesema kuna deal kubwa la mamilioni ya fedha kutoka kwa kampuni inayotaka kuchukua nafasi ya Nike kama mtengenezaji wa mavazi ya michezo ya Pacquiao.

Pineda pia alidai kuwa hakuna kampuni ya Ufilipino iliyovunja mkataba wa udhamini na Pacquiao kufuatia kauli yake hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents