Burudani ya Michezo Live

Makamu wa Rais alivyouzungumzia wimbo wa Diamond “Mkisema CCM Baba lao, Wataweza kweli…! aaah wapi….! isiwe mdomoni tu” – Video

Makamu wa Rais alivyouzungumzia wimbo wa Diamond "Mkisema CCM Baba lao, Wataweza kweli...! aaah wapi....! isiwe mdomoni tu" - Video

Mamamu wa rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan alipata nafasi ya kuongea na kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha miaka 43 ya chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dar Es Salaam pia akiwa kama mlezi wa chama hicho kwa mkoa wa Dar Es Salaam.

Akiongea mambo mengi kuhusu Chama hicho aliwaasa Wana CCM kuwa na mapenzi na kufuata itikadi za Chama, Lakini pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa wanaCCM ambao wameanza kujipitisha majimboni kwa lengo la kuwania ubunge kwenye majimbo hayo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Mbali na hilo aliwapa tahadhari wale wanaowatimua baadhi ya wanachama wa CCM wakitoa madai mabalimbali  “Msitupunguzie mtaji mapema hivyo kwa sababu mkisimamisha watu sasa hivi, mkifukuza watu sasa hivi, kila mnayemfukuza ana ndugu, jamaa na marafiki, watamuunga mkono kwenye nongwa yake aliyo nayo, kwa nini mtengeneze nongwa sasa hivi?” “Uchaguzi uliopita hizi ndizo fimbo tulizojipiga wenyewe, watu wanatosha tukaandika hawatoshi, wengine wakakatwa ovyo wakanuna wakaenda upande wa pili wakaenda kutuharibia,”

Makamu wa Rais pia aliwataka wanaCCM wanaopenda kuutumia wimbo wa Baba lao wa Diamond Platnumz huku wakisema “wataweza kweli…! aaaah wapi…..! huku wakiongea pasipo kutoa kauli hizo ndani ya moyo wao na badala yake wakiongea mdomoni tu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW