Habari

Makamu wa Rais amfagilia Rais Magufuli nchini Mauritania (+video)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amesema “Tanzania chini ya Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inajitahidi sana kupambana na rushwa pamoja na viashiria vyake”.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kujadili Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2018 “Kushinda Vita dhidi ya Rushwa: Njia endelevu ya mabadiliko ya Afrika” katika Mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaomalizika leo mjini Nouakchott, Mauritania.

Makamu wa Rais amesema rushwa inaumiza watu hususani watu masikini na kudhoofisha ukuaji wa uchumi hivyo ni vyema rushwa ipingwe kwa nguvu zote.

Aidha, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatambua vita dhidi ya Rushwa inahitaji jitihada za pamoja katika ngazi zote ikiwemo Kitaifa, Kikanda na Bara zima.

Katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbali mbali, Tanzania itaendelea kushiriki katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents