Habari

Makamu wa Rais aongoza kuuaga mwili wa mke wa Waziri Mwakyembe

Viongozi mbalimbali wamejitokeza katika ibada ya kuuaga mwili wa mke wa Waziri Mwakyembe aliyefariki Jumamosi iliyopita katika hospitali ya Agha Khan alipokuwa akipatiwa matibabu.

Ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT ushirika wa Kunduchi baada ya kuaga hapo umesafirisha kuelekea Kyela jijini Mbeya ambapo ndipo utakapo pumzishwa mwili wa Bi Linah Mwakyembe.

Viongozi mbalimbali wamehudhulia ibada hiyo akiwemo, Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suzan Kolimba, Kamanda wa zamani wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, Katibu Mkuu CCM, Abdurahman Kinana, Katibu Muenezi CCM, Humphrey Polepole,Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu na baadhi ya wasanii.

Akiongea kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Rais Magufuli tayari ameshatoa salamu za rambirambi huku akisema Rais amesikitishwa na msibva huo alkadhalika ametoa pongezi kwa Dkt Mwakyembe ambapo pamoja na kumuuguza mkewe hakuacha kutimiza majukumu yake ya kiserikali.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents