Habari

Makamu wa Rais atoa agizo kwa IGP, Sirro (+video)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo, wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents