Shinda na SIM Account

Makamu wa Rais atoa agizo wakati wa uzinduzi kampeni ya usafi wa mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ameagiza utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira uwe ni ajenda ya kudumu ya kila ngazi ya Uongozi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira awamu ya pili, iliyozinduliwa rasmi kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Chang’ombe mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya Pili ukiofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe,mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais alisema Serikali imejiwekea mikakati mbali mbali ya kupambana na maradhi ya kuambukiza ambapo usafi wa mazingira ni njia mojawapo ambapo katika awamu ya kwanza ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira ambapo jumla ya kaya 1,662,550 zilijengwa vyoo na shule 2,133 vilijengwa vyoo bora.

Katika awamu ya Pili iliyozinduliwa leo Kaya 5,600,000 zinatarajiwa kuongeza idadi ya vyoo bora na shule za msingi 3,500 na sekondari 700 zitapata huduma ya vyoo bora na sehemu maalum ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.

“Wahenga walisema Samaki mkunje angali mbichi, methali hii inatukumbusha jukumu la kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa usafi wa mazingira tangia wadogo wakiwa mashuleni”alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alitoa Wito kwa Wanawake wote nchini kujifunga Kibwebwe na kujenga vyoo, alisema Wanawake wamekuwa na vikundi mbali mbali vya kusaidiana na kuwezeshana hivyo kwa kupitia vikundi hivyo wanaweza kufanikisha ujenzi wa vyoo bora majumbani.

Makamu wa Rais aliwapongeza Washindi wote wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2016/17. Pia aliwashukuru wadau mbali mbali ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine kufanikisha uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW