Habari

Makamu wa Rais aziagiza halmashauri kujenga nyumba za watumishi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameziagiza halmashauri zote nchini kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa afya hasa katika maeneo ya vijijini, akisisitiza kipaumbele kitolewe kwa wakunga ambao wanatoa huduma za dharura wajawazito.

Bi Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika siku ya maadhimisho ya ‘Siku ya Wakunga’ duniani ambapo amesema kuwa halmashauri zijenge nyumba karibu na vituo vya afya.

Mheshimiwa Samia alisema “Baadhi ya watumishi wa afya hasa wakunga wanakaa mbali na maeneo yao ya kazi, hivyo kusababisha utoaji wa huduma za dharura kuwa duni hivyo nawahimiza Wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ujenzi huo kikamilifu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi nchini.”

Makamu wa Rais amewahimiza wakunga kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili huku akiwataka waache tabia ya kutoa lugha mbaya kwa wanawake wajawazito.
Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents