Promotion

Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika kitengo cha Mawasiliano atembelea Tanzania

By  | 

Makamu wa raisi wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano kwa umma (katikati pichani), leo amepongeza juhudi za wanahabari nchini mara ya kutembelea baadhi ya vyombo vya habari Tanzania, ikiwemo IPP media na Mwananchi Communication, ikiwa ni ziara ya siku mbili ya aliyojiwekea ili kujionea mambo mbalimbali katika ulimwengu wa Habari na Mawasiliano nchini.

Akiongea wakati wa ziara hiyo akiwa na wadau mbalimbali na wanahabari Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika bw, Michael Okwiri alisema “Nimegundua Tanzania kunamaendeleo mazuri sana hasa ukiangali mitambo na vyombo vya habari kwa kweli vinaonyesha kupiga hatua kwa kiwango. Vilevile nawapongeza sana wanahabari (Journalists) kwa juhudi zenu za kutafuta habari na kuziwahisha kuzichapa kwa muda wa siku pamoja na mambo mengi, kwa kweli ni juhudi inayohitajika kukamilisha mambo haya mapema ili wasomaji wapate taarifa inayoendana na muda Kwa upande wetu, Airtel, naomba niwashukuru wanahabari wote kwa ujumla nchini Tanzania hasa mnaoshirikiana nasi Airtel kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya uhakikika inawafikia wananchi kwa kupitia baadhi ya habari zinazochapwa na kusambazwa nchini na vyombo vyenu. Airtel tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mawasiliano ili tuweze kutimiza dhamira yetu ya Uhuru wa kuongea nchini kote” alimaliza kwa kusezema Bw. Okwiri

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments