Makamuzi bado yanaendelea UK-Jide

Judith Wambura a.k.a Binti Machozi a.k.a Lady JayDee kama unahofia kuchapia waweza kumuita Jide, bado anaendelea na ziara yake nchini uingereza ambapo anatarajia kupiga show nyingine mbili kabla hajarejea…

jaydee_jap_l.jpg

 

Judith Wambura a.k.a Binti Machozi a.k.a Lady JayDee kama unahofia kuchapia waweza kumuita Jide, bado anaendelea na ziara yake nchini uingereza ambapo anatarajia kupiga show nyingine mbili kabla hajarejea, kesho atakuwa Club Afrique jijini London wakati Juma Mosi atakamua ndani ya Birmingham.

Jide ambaye kwa sasa yupo katika mji wa Manchester alizungumza na bongo5.com kwa njia ya mtandao na kusema kuwa anatarajia kutua bongo mara tu baada ya kumaliza show hizo mbili ambazo zimeandaliwa na watanzania waishio huko.

“Huwa naamini jitihada pekee ndio zinaweza kumfanya msanii kufikia hapa ambapo mimi nimefikia, so napenda mashabiki wasidhani nimewasahau namalizana na hivi vimeo then Ijumaa Machozi Band kama kawa katika viwanja vya zamani kwani nitatua bongo tarehe 10” alisema Jide.

Hii inaonesha wazi kuwa oneho ambalo ndio lilikuwa sababu ya Jide kwenda UK limezaa maonesho mengine mawili, “Yeah nilikuja tu kwa ajili ya Mandela lakini nimeweza kukutana na show nyingine mbili, sasa hii ni kazi yangu hivo ningependa ifahamike kuwa makamuzi bado yanaendelea pande hizi”-Lady Jay Dee.

Mwanadada huyu anatamba sana na ngoma zake ambazo zimekuwa zikiwashika mashabiki wa muziki wa Tanzania ulimwanguni, alijipatia bahati ya kwenda kufanya onesho katika sherehe ya kuzaliwa Raisi wa zamani wa Afrika kusini mheshimiwa Nelson Mandela iliyofanyika nchini Uingereza wiki iliyopita.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents