Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Makande yampa mafanikio mpiga kura Kenya

Mwanaume mmoja nchini Kenya, Martin Kamotho baada ya picha yake kusambaa katika mitandao ya kijamii akiwa kwenye foleni ya kuelekea kumchagua Rais wa Kenya, huku akiwa na mfuko wa makande mkononi ameibuka shujaa kupitia kitendo hicho.

Picha ya Martin maarufu kama Githeriman, ilisambaa na kupelekea apate mafanikio kwa kuzawadia vitu mbalimbali kama vile-: Sehemu ya bure ya kuishi katika maeneo ya Karen, Smart phones ya bure aina ya Samsung S8 iliyotolewa na kampuni ya Safaricom huku watoto wake wakipewa simu aina ya Tecno Canon.

Pia amepatiwa nafasi ya kwenda mapumziko na familia yake katika maeneo ya kivutio yaliopo Kenya, Maasai Mara na Kampuni moja ya kitalii ndiyo imehusika kusimamia mchongo mzima. Vile vile amepatia nguo za bure na duka moja la suti lilopo nchini humo.

Githeriman ameonekana kufanya kitendo cha kishujaa kwa kushiriki uchaguzi huo amabo ni muhimu huku akiwa ana kula jambo ambalo mtu mwingine asinge weza kula hadharani kwa kuhofia kupata aibu ama kuonekana.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW