Habari

Makonda alipiga teke swali la vyeti ‘maswali ya mtandaoni yanaishia huko’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala la kughushi vyeti kwasababu majibu yake yapo mtandaoni suala hilo lilipoanzia.

Makonda amesema hayo Ijumaa alipoulizwa swali na mwanahabari wa Bongo5 (Yasin Ngi’tu) kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.

“Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye madawa ya kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,” alisema.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents