Habari

Makonda amuonesha magufuli jipu la Ubungo

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kuna wizi mkubwa alioubaini unaoendelea kufanyika kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo.

Makonda

Makonda amesema hayo alipokuwa akitoa salamu za Mkoa wake wa Dar es Salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni (Nyerere).

“Mheshimiwa Rais kutokana na kamati ya uchunguzi niliyoiunda ilibaini kuwa katika stendi ya mabasi ya Ubungo, kumekuwa na ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma, ikiwemo kutokuwasilishwa kwa mapato halisi yanayotokana na makusanyo ya kila siku serikalini,” alisema Makonda.

Mhe. Makonda aliendelea, “Kamati ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine mwaka 2009 kwa lengo la kunufaisha wachache.”

Aidha Makonda amefafanua kuwa Sheria Ndogo ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato ndani ya kituo hicho, inaonesha kuwa kila basi linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo.

Aliongezea kuwa, “Kutokana na mabadiliko ya tozo, sheria hiyo ilibadilishwa mwaka 2009 na kila basi likatakiwa linatozwa Sh 8,000 na hivyo makusanyo ya mwezi yakapanda na kufikia Sh milioni 82 kwa mwezi jambo ambalo halikufanyika kwa kipindi chote kwa kutekeleza sheria ya mwaka 2009 hivyo tunapoteza milioni 500 kwa mwaka kwa hesabu za haraka haraka.”

Hata hivyo Makonda amesisitiza kwamba tayari amewasilisha suala hilo kwa taasisi ya kupambana na rushwa nchini TAKUKURU kwa ajili ya kufanya kazi yao ili wote ambao walihusika kuipotezea serikali mapato wachukuliwe hatua stahiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents