Habari

Makonda awakumbusha watanzania umuhimu wa michezo

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewakumbusha watanzania umuhimu wa sekta ya michezo na sanaa. Amewataka kushiriki katika fursa mbalimbali za kimichezo zitolewazo.

watsap-cover-1848

Ameyasema hayo katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa tuzo mbalimbali kwenye kilele cha michuano ya gofu ya mkuu wa majeshi iliyofanyika kwenye viwanja vya klabu ya gofu ya Lugalo

“Kwetu sisi michezo inaua ukabila, kwetu sisi michezo inaua udini, kwetu sisi michezo inarejesha amani, upendo na umoja katika taifa letu, kwahiyo hatuna budi kuendeleza na kuwapongeza waasisi wote wa michezo mbalimbali waliyoianzisha ndani ya nchi yetu na mikoa yetu, kupitia michezo hiyo inatupa faraja na kutujenga zaidi,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alisisita kuwa mbali na kuwa michezo ni afya pia michezo husaidia kudumisha amani na mshikamano baina ya jamii hivyo ni vyema watu wakashiriki michezo pale fursa zinapojitokeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents