Habari

Makubaliano ya kuweka silaha chini kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza bado kiza kinene

Makubaliano ya kuweka silaha chini kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza bado kiza kinene

Makubaliano ya kuweka silaha chini kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza yanasuasua, huku kukiwa na ripoti za jeshi la Israel kumpiga risasi kwa kijana mmoja wa Kipalestina. Jeshi la Israel linasema limempiga risasi na kumteka Mpalestina mmoja aliyekuwa akikaribia kwenye uzio wa Gaza huku akirusha mabomu ya mkono kuelekea upande wa Israel.

Kwa mujibu wa DW Swahili, Tukio hili la leo (Jumatano 14 Novemba) ni la kwanza tangu Hamas na makundi mengine ya wanamgambo kwenye Ukanda wa Gaza kusema wamekubaliana na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Misri ili kukomesha siku mbili za mapigano makali ambayo yamewaweka mahasimu hao wawili kwenye ukingo wa kutumbukia vitani.

Jeshi la Israel linadai liligundua kuwa mshambuliaji huyo alikuwa na kisu na mkasi wa kukatia nyaya za uzio huo. Hata hivyo, kwa mujibu wa jeshi hilo, mabomu aliyoyarusha hayakuripuka.

Hayo yakijiri, kikosi kinachosimamia mapigano hayo kwa upande wa Israel kimeondoa vizuizi kwa wakaazi wa kusini mwa nchi hiyo na watoto wameanza kuenda skuli leo.

Kundi la Hamas limesisitiza kuwa litaendelea kuyaheshimu makubaliano hayo kadiri ambavyo upande wa Israel nao utafanya hivyo.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman ataka mashambulizi yaendelee

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman, anayetambuliwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya Wapalestina, alisema hapo jana kwamba haungi mkono wazo la kuacha mashambulizi. Anatazamiwa kutoa kauli rasmi jioni ya leo.

Jeshi la Israel linadai kuwa wanamgambo wa Kipalestina walirusha makombora 460 kuelekea Israel ndani ya kipindi cha masaa 24, nayo Israel ikifanya mashambulizi 160 ya anga kulenga maeneo mbalimbali ya Gaza. Kwa ujumla, Wapalestina saba, wakiwemo wapiganaji watano, wameuawa tangu kuanza kwa mapigano hayo, huku Israel ikipotea raia wake mmoja aliyeuawa kwa roketi na wengine 27 wakijeruhiwa, watatu wakiwa na hali mbaya sana.

Mapigano haya yaliyochukuwa siku moja tu yanatajwa kuwa mabaya kabisa tangu vita vya mwaka 2014. Mashambulizi ya anga ya Israel kuharibu majengo kadhaa na kuligeuza anga la Gaza kuwa jeusi kwa moshi na moto.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents