Burudani

Makundi matano ya Bongo Flava yaliyoacha historia

Zamani Bongo Flava ilitawaliwa na makundi mengi mno pengine kutokana na wasanii hao kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kwenda studio mmoja mmoja basi njia nzuri ilikuwa ni kujikusanya kwenye makundi huku wakichanga hela mpaka zilipofika senti za kwenda kuwaona akina Master Jay,Mika Mwamba ama P- Funk Majani.

majanibc
P-Funk Majani anafahamika kama Godfather wa Bongo Flava

Makala hii inakuletea makundi matano bora yaliyowahi kufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Flava.

Daz Nundaz Family

daznundaz

Hit kama Maji ya Shingo,Kamanda na Barua zililifanya Daz Nundaz liwe kundi bora zaidi kwenye Bongo Flava kwa wakati ule. Ungesema nini kuhusu sauti ya kulalamika ya Ferooz? Bila kumsahau Fundi Daz, Mwalimu,Lusajo,La Rhumba na Critic.

Kamanda ni ngoma iliyowafanya watu wawatolee macho kwa makini ila Barua ilimaliza kila kitu.

Kwa sababu ambazo hazijawahi kuwa wazi pengine maslahi,ushauri mbaya au kujiona bora kuliko wenzie kwenye kundi, waliishia kutoa album moja tu, Maji ya Shingo, kabla ya Ferooz kujitoa na kwenda kufanya ngoma kali kama Jirushe,Umeniponza na wimbo wa taifa, Starehe aliomshirikisha Profesa Jay.

Baadaye Daz Mwalimu aligeuka Daz Baba na kukutana na Fid Q na kufanya wimbo, Namba 8 kabla ya kukutana na marehemu Ngwea kutengeneza wimbo mwingine wa taifa, Wife.

Wenzao waliobaki kwenye kundi hawakuwa na nguvu kama waliojitoa na mwisho wa siku kundi likafa huku kila mtu akilitamani.

Wakajaribu kurudi tena baada ya miaka kadhaa na nyimbo kama Jahazi la Daz na Nipe 5 lakini hawakudumu kabla ya kila mmoja kwenda na njia yake. Wengine hawajulikani walipo ila Ferooz na Daz Baba bado wanajikongoja.

Solid Ground Family

https://www.youtube.com/watch?v=jANqdSdaVJQ

Unaukumbuka wimbo wa Bush Party? Ile party ambayo Muhogo Mchungu alicheza na mbuzi? Yeah ile party ambayo jamaa aliingia na ngedere na kuzua kitimtim kikubwa humo mpaka walipomtoa na ngedere wake ndipo utulivu uliporejea mahala pake! Naam.

Achana na Mechi Kali, kati ya timu ya Kifo na timu ya Uhai, mechi ambayo timu ya kifo ikiongozwa na striker wao mkali UKIMWI alipomtungua kwa ufundi mkubwa kipa Panadol wa timu ya UHAI.
Hawa jamaa pia walitupa story kali kama ATHUMANI AKISHALEWA anavyoshindwa kujielewa. Ulikuwa wimbo mkali wenye ujumbe kuhusu matumizi ya pombe kupitiliza yalivyo na madhara.

Hawakuishia hapo, walileta pia wimbo mzuri mno wa BABA JENI alivyopata mafao tabia yake ilivyobadilika kuwa kituko mtaani.
Kichaa cha Jerry ilikuwa ngoma nyingine kali kutoka kwao ambao ulielezea kwa kirefu ubaya wa matumizi ya bangi ambayo ilimpelekea mshkaji wao JERRY kupata ukichaa kama utani.

Ghafla Jerry alivaa shuka na kujiita shetani na sometimes alivaa majani na kujiita yeye nyani.

Solid Ground Family walikuja na style fulani ambayo ilikuwa na visa vingi ndani yake vilivyokuwa vinaiasa jamii kujiepusha na starehe zisizo na lazima.

Hatujui nini kilitokea, tunachojua jamaa walipotea kama utani huku nyimbo zao zikiendelea kuwa na mafunzo mengi na makubwa mpaka kesho. Hakuna yoyote kati yao alieweza kuhit nje ya kundi.

2 Berry

https://www.youtube.com/watch?v=WyqKla66Tlc

Berry Black na Berry White – washkaji kutoka Unguja. Walikuwa pamoja toka utotoni na walikuwa kama ndugu ila wimbo mmoja tu wa NATAKA KUWA NA WEWE ulivuruga kila kitu kizuri walichokitengeneza miaka yote.

Berry Black aliona Berry White anajifanya staa kisa aliimba sehemu kubwa kwenye wimbo ule kitu ambacho Berry Black hakupendezwa nacho na kumuonyesha Berry White kuwa yeye ni mkali zaidi yake alimtafuta Suma Lee na kufanya naye wimbo wa NISAMEHE ambao ulifanya kundi lao kuvunjika huku likiwa bado la moto pamoja na juhudi za ndugu zao kuwapatanisha na kuwakumbusha walipotoka, haikuwa kitu rahisi kumrudisha Berry Black kwenye utawala wa Berry White.

Berry Black bado anafanya poa huku wimbo wa mwisho wa ISHARA ZANGU aliofanya na Ali Kiba ukizidi kumsimamisha kisanii ila mwenzake Berry White yupo nje kabisa ya game na ameshindwa kabisa kusimama mwenyewe toka kundi lao livunjike.

Parklane

https://www.youtube.com/watch?v=mKB5XdON6Ck

Washkaji kutoka Tanga kule kule wanapotoka wakali wa mapenzi.
Ilunga Khalifa au Computer Programmer, muite mwite CP kwa kifupi mzee wa Crunk na mwanae Suma Lee waliunda kundi moja kali kwenye Bongo Flava, Parklane.

Nyimbo zao nyingi walizifanyia kwenye studio za Mombasa.

Ngoma kama Aisha Aisha,Nafasi Nyingine zilikuwa ngoma kali mno kutoka kwao ila kama utani Suma Lee alipotoka na wimbo wa Chugwa akiwa peke yake huku ikifuatiwa na wimbo wake mwingine, RAFIKI ambao ulisemekana kuwa ni dongo kwa CP.

Ushkaji wao ukaishia hapo, CP akarudi pia akiwa peke yake na ngoma zake za PWAA kwa style yake ya CRUNK.

Suma Lee bado yupo kwenye game huku wimbo wake wa taifa HAKUNAGA ulimrudisha baada ya kupotea kwa kipindi kirefu. Baada ya hapo aliachia ngoma zingine kama tatu ambazo hazikufanya vyema. Kwa sasa yupo tu akifanya biashara zake na kwa wale wanaomfuata Instaram watagundua kuwa miaka ya hivi karibuni amekuwa mshika dini ya Kiislamu mzuri.

Cpwaa ameendelea na harakati nyingi za muziki ikiwa ni pamoja na kuachia ngoma mpya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita zikiwemo Chereko Chereko na Kata Kiu. Pia alianzisha label yake iitwayo Brainstorm Music na kuwasainisha Wadananda.

Gangwe Mobb

gangwe_sim

Wazee wa Rap katuni kutoka Temeke Mikoroshoni. Ungesema nini kuhusu Inspector Haroun wa wakati ule! Wimbo kama Mtoto wa Geti Kali ingekupa simulizi nzuri ya mtoto wa uswahilini uswazi anayemzimikia mtoto wa geti huku akishindwa kumchana ukweli na kubaki na kigugumizi pale mtoto anapomwambia sema basi unataka nini.

https://www.youtube.com/watch?v=hUXofweH4t8

Walikuwa wapo vizuri mno na kwa hakika walikuwa kundi bora la Bongo Flava kwenye zama zao. Ungebisha nini kama ulikuwepo wakati ule na ungeusikia wimbo wa NJE NDANI ambao majamaa waliwachana washkaji waliozamia mtoni huku wakigoma kurudi Bongo zaidi ya kuwatumia picha tu na email zisizo na msingi mwisho wa siku visa inachwana huku passport ikipigwa X.

Leo wapo kama wapo. Aliyekuwa anaonekana baba wa kundi Inspector Haroun aliamua kujitegemea na kuachia ngoma kali kama Asali wa Moyo na Bye Bye. Hata hivyo Luteni Kalama hakuwa kuhit akiwa solo artist kama mwenzake. Usijaribu pia kuusahau ushirikiano wa Inspector na Sir Nature uliozaa remix kali ya Mzee wa Busara.

Imeandikwa na Heri Athumani ([email protected]). Editing and additional content by Fredrick Bundala

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents