Habari
Makusanyo ya kodi yaongezeka asilimia 1.2
Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa ripoti ya makusanyo ya kodi ya kipindi cha kwanza cha robo ya mwaka wa fedha wa 2017/18, ambapo kuanzia mwezi Julai hadi septemba Serikali imekusanya kiasi cha Tsh Trilioni 3.65 .
Makusanyo hayo kwa miezi mitatu ni sawa na ongezeko la asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha wa 2016/17.
Makusanyo ya kodi ni kama ifuatavyo.
Mwezi Julai – Tsh trilioni 1.1
Mwezi Agosti- Tsh trilioni 1.2
Mwezi Septemba- Tsh trilioni 1.3