Burudani

Malaika afunguka kuhusu kashfa ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja (Video)

Msanii wa muziki, Malaika aka Queen Malaika, amefunguka kuzungumzia kashfa nzito iliyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa aliwekwa kinyumba Marekani na mwanamke mwenzake.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Zogo’ alifanya tour ya miezi mitano ya muziki wake nchini Marekani ndipo tetesi hizo zilivyoanza kuzuka baada ya kuonekana kuwa karibu na mama mmoja aliyemzidi umri.

Mama huyo alionekana kupost picha nyingi za muimbaji huyo kupitia mtandao wake Instagram hali ambayo ilifanya tetesi hizo kuwa kubwa zaidi.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Malaika amekanusha uvumi huo huku akidai yule mama ambaye anaonekana kuwa naye karibu ni mtu anayemuheshimu huku akidai anamchukulia kama mama yake.

“Yule ni mama yangu, ni mtu ambaye namuita kama mama yangu kwa sababu ni mtu ambaye ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wangu. Kwahiyo amenizidi umri na ni mkubwa sana na namuheshimu sana, na namuita kama mama so sidhani kama mama yako mnaweza mkafanya michezo ya ajabu,” alisema Malaika.

“Haya yametokea kwa sababu toka niachane na aliyekuwa mpenzi wangu wahajawahi kusikia ninatoka na nani, wala hawajawahi kuniona hata nimekaa na mtu fulani, wakahisi mambo kama hayo. Kwahiyo wajue mimi sio mtu wangu na sijalelewa kwenye mazingira ya kufanya vitu kama hivyo,” aliongeza Malaika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents