Burudani

Malaika bado yupo yupo sana kwenye muziki

Yupo wapi Malaika? Hilo ndio swali wanalojiuliza mashabiki kwa sasa.

Hitmaker huyo wa Rarua, amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, yupo Marekani kwa ajili ya ziara zake za kujitangaza zaidi kimataifa kwenye muziki.

“Sijaacha muziki ila kwa sasa nipo nchini Marekani kwa ajili ya tour yangu ya kimuziki ambayo ninaanza kujitambulisha kimataifa lakini nitakapomaliza nitarudi nyumbani kuendelea na kazi zangu. Siwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja ikiwemo kufanya tour na huku kuachia ngoma kwa wakati mmoja,”amesema Malaika.

Kila mtu ana uwezo wake wa kuhandle vipi vitu vyake lakini kwangu mimi natakaga kufanya kitu kimoja kwanza halafu ndio nifanye kitu kingine,” ameongeza. Muimbaji huyo amesisitiza yapo mengi zaidi yanazungumzwa juu yake lakini hayo yote hayana ukweli wowote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents