Michezo

Mali mabingwa wapya fainali za U 17 Gabon

Timu ya taifa ya vijana ya Mali iliyo chini ya umri wa miaka 17 imetwaa Ubingwa wa michuano ya AFCON hapo jana baada ya kuifunga timu ya Ghana kwa jumla ya magoli 2- 1 nchini Gabon

Mali, imeibuka na ushindi huo mwembamba katika mchezo ulio kuwa na upinzani mkubwa kwa pande zote mbili kuhitaji kuchomoza na ushindi , na hatimae timu hiyo ilipata goli la pekee kupitia kwa mchezaji wake Momadou Samake , lililo dumu hadika dakika 90 za mchezo.

Baada ya kuingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, kocha wa Ghana Paa Kwesi Fabin alipanga kikosi chake cha kwanza ambacho kiliifunga Niger 6-5 katika hatua ya penati  kwenye hatua ya nusu fainali.

Ghana walianza kwa kasi kipindi cha kwanza baada ya Eric Ayiah kupata nafasi ya wazi lakini hakuweza
kufunga

Kocha wa Ghana Ghana Paa Kwesi Fabin amesema pamoja na kupoteza mchezo huo, wachezaji wake walifanya jitihada za kutosha ila bahati haikuwa upande wake.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents