Michezo

Mali na Ghana zatinga fainali ya U17

Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.


Wachezaji wa Ghana wakishangilia baada ya mchezo kumalizika

Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

Mabingwa watetezi Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali, Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati


Wachezaji wa Timu ya Mali wakishangilia

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la AmitiƩ Sino-Gabonaise, mjini Libreville,

Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa AmitiƩ Sino-Gabonaise.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents