Burudani ya Michezo Live

Malinzi akumbana na rungu la FIFA, Apigwa kifungo miaka 10 na faini juu

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemfungia miaka 10 aliyekuwa Rais wa
TFF, Jamal Malinzi kutojihusisha na soka, Baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.

Jamal Malinzi

Fifa wamesema Malinzi alipokea Dola $528,000 sawa na Tsh. Bilioni 1 ukiwa ni mkopo wa miaka minne aliyokuwa madarakani, lakini alishindwa kutoa taarifa ya matumizi ya fedha za mkopo huo.

Taarifa hiyo ya FIFA, Imeeleza kuwa Malinzi pia alipokea dola $55,000 sawa na Tsh. Milioni 126 fedha ambazo zilikuwa ni zawadi kwa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U17 kwa kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon.

Mbali na kifungo hicho, Malinzi pia kapigwa faini ya dola $503,000 sawa na  Tsh Bilioni 1.1 .

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW