Michezo

Malinzi atuma salamu za rambi rambi msiba wa Ally Yanga

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Jamal Emil Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa uongozi wa klabu ya Yanga SC, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Ally Yanga ambaye amefariki dunia Juni 20 mwaka huu.

Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa Young Africans, Ally Mohammed anayefahamika zaidi kwa jina la Ally Yanga, kilichotokea jana Jumanne Juni 20, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Dodoma.

Katika salamu za rambirambi kwa uongozi wa Young Africans, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Ally Yanga ambako Rais Malinzi amewaasa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao na kwa huzuni amewafariji akisema: “Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea.”

Mwanachama wa Yanga SC aliyefariki dunia maarufu kwa jina la , Ally Yanga

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents