Michezo

Malinzi na Mwesigwa kuendelea kusota rumande hadi Agosti 24

Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa imehairishwa mpaka Agosti 24 mwaka huu ambapo watarudishwa tena Mahakamani kusomewa mashtaka yao.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea kusomewa mpaka sasa.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko amedai kwamba inaonyesha vielelezo tayari vimeshafikishwa Mahakamani lakini upande wa mashtaka unachelewesha kutolewa uamuzi.

Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents