Michezo

Malinzi na wenzake ngoma bado nzito

By  | 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerejeshwa tena mahabusu hadi Julai 31 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa

Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea mpaka sasa.

Mnamo Juni 27 mwaka huu, Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.

By Hamza fumo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments