Habari

Mama aliyejifungua mapacha wa baba wawili tofauti azua gumzo

Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Bi, Rashida Nakabugo nchini Uganda, amejikuta akiingia kwenye gumzo kubwa baada ya kutoka kwa vipimo vya vinasaba (DNA) vinavyoonesha kuwa watoto wake mapacha waliyokuwa wakigombaniwa na wanaume wawili kwa zaidi ya miaka mitatu toka kujifungua kwake kila mmoja ana baba tofauti badala ya kuwa wa mtu mmoja kama ilivyozoeleka.

Ssegane (wapili kutoka kushoto) mwenyeshati jekundu,Bi  Nakabugo (katikati) na Ssengendo (wakulia) mwenyeshati jeupe

Miaka mitatu ya mgogoro wa wanaume hao ambao waliyokuwa wana wapigania mapacha hao waliyofahamika kwa jina la Babirye na Leticia Nakato umemalizwa kwa kila mmoja kupata mtoto mmoja kufuatia matokeo hayo ya vinasaba yaliyotolewa na kituo cha Health Viber Diagnostics huko Kampala nchini Uganda.

Vipimo hivyo vya DNA vimeonyesha kuwa, Babirye ni mtoto wa Baseka Sengendo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Mpigi na Leticia Nakato ni wa Patrick Ssegane mwenye umri wa miaka 30 licha ya kuzaliwa siku moja na mama mmoja.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha New Vision kimeeleza kuwa wanaume wote wawili wanaamini kila mmoja ndiye mzazi sahihi wa mapacha hao Babirye na Leticia Nakato.

Duru ya habari inasema kuwa Ssengendo ni mume halali wa mama huyo, Nakabugo ambaye pia kwa wakati huo mwanamke huyo alikuwa na mahusiano na Bw, Ssegane.

Mume wa Rashida Nakabugo, ambaye ni Ssengendo amesema kuwa wakati mkewe anajifungua hakuwepo nyumbani.

Wakati kwa upande wa Ssegane amesema kuwa alimkubali mama huyo baada ya kutengana na mumewe hata hivyo baada ya woto kukua mara kadhaa amekuwa akihitaji kujua ukweli kuhusu mapacha hao.

Chombo cha habari cha Azam tv hapa nchini kimeripoti kuwa Madaktari baada ya kupata matokeo ya vipimo kuwa ni watoto wenye baba wawili tofauti walivipeleka huko Ohio nchini Marekani (USA) na kuhakiki matokeo hayo na kusema inawezekana.

Maamuzi yaliyofikiwa baada ya matokeo ya habari hiyo ya kushtusha na iliyozua gumzo kubwa nikuwa Ssengendo ameridhia kumuachia watoto wote wawili Ssegane ambaye yeye ndiye aliye leta wazo la kufanyika kwa vipimo hivyo vya vinasaba (DNA) kwakuwa amekuwa akiishi na mwana mke huyo na watoto hao kwa muda wote huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents