Habari

Mama aporwa mtoto wake mikononi na mnyama Chui akiwa ndani ya gari

Mama aporwa mtoto wake mikononi na mnyama Chui akiwa ndani ya gari

Mama mmoja nchini India anayetambulika kwa jina la Sapna amejikuta akiingia kwenye vita kubwa ya kumtetea mtoto wake wakiume Ayush baada ya chui kumvamia alipokuwa kwenye gari na mumewe kisha kumpora mtoto huyo akiwa mikononi mwake.

Image result for Leopard attacks couple in Gujarat, snatches infant

Mume wa Sapna ambaye ni Vikram Rathwa amesema kuwa mkewe na mtoto wake Ayush wamepata majeraha makali katika purukushani hizo na kuwaishwa hospitali huko magharibi mwa India Gujarat.

Rathwa ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi kwenye kijiji cha Raipur huko Pavi Jetpur nchini India ambapo wananchi walijitokeza na kumfukuza chui huyo baada ya kupiga kelele ya kutaka msaada.

Taarifa zinaeleza kuwa wote watatu wamechukuliwa na kufikishwa kwenye hospitali ya Shri Sayajirao General huko Vadodara huku daktari akisema kuwa mama wa mtoto Ayush amejeruhiwa kwenye mgongoni na eneo la nyuma ya magoti.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents