BurudaniDiamond Platnumz

Mama Ashura adai Alikiba anamuhofia Diamond

Muigizaji kutoa Timamu Africa Media, Mama Ashura amedai kuwa msanii Alikiba anamuhofia Diamond Platnumz na ndio sababu ya kuchelewa kutoa wimbo.

Mama Ashura na Ebitoke

Mama Ashura ambaye amekuwa akiigiza mara nyingi na Ebitoke, amekiambia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm kuwa Alikiba ana kipaji kikubwa lakini ameshindwa kukifanyia kazi kwa sababu ya hofu.

“Anamuhofia halafu ukifanya kitu kwa kumuhofia mtu that means hutakuwa makini katika kazi yako, kitu ambacho unatakiwa ufanye ni kujiamini wewe kama wewe katika nafasi yako halafu pokea ushauri wa watu. Hamna mtu ambaye amezaliwa anajua kila kitu na sio kila ushauri ni mzuri pia, lakini angalia, haiwezekani watu 10 wanakushauri kitu halafu wewe unakuwa na wazo la tofauti, haiwezekani,” amesema Mama Ashura na kuongeza.

“Kwa hiyo kitu ambacho nakiona ni kwamba ajiamini yeye kama yeye na nanfasi yake na sauti yake, awasikilize masabiki wake na hiyo fan base kubwa ambayo anayo aifanyie kazi ili tuone utofauti ambao upo,” amesisitiza.

Hata hivyo muigizaji huyo hakusita kueleza hisia zake kwa Diamond, “To be honest Diamond namuelewa sana anavyoimba, kingine ninachomuelewa zaidi aisee anajituma. Unajua mtu ukishatoka katika maisha fulani ukayahofia ina maana utajituma utaki kuyarudi, kwa hiyo anajituma zaidi ya Alikiba ambaye kipaji chake ni kikubwa lakini hajitumi.

“Ukisema wewe una kipaji forever halafu haukitendei haki halafu akaja mtu ambaye hana kipaji lakini akajituma mpaka akaingia katika level zako na kuzipita, that means huyo mtu anajituma zaidi yako,” amesema Mama Ashura.

Kwa upande waka Ebitoke amejinadi kuwa yeye ni team Kiba na kumshauri msanii huyo kitu cha kufanya wakati huu.

“Ndiyo mimi ni team Kiba, cha kumshauri Kiba wangu atoe wimbo mpya ili tuwakomeshe hao wakina Mama Ashura na team Diamond.  Alikiba anakuja na kitu ambacho kitasimama fire. Nakuamni Kiba wangu na ninakujua kwenye muziki haupo vibaya, wewe unaimba, una vocal toa wimbo mwingine ili watu waone,” amesema Ebitoke.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents