Habari

Mama atapeliwa nyumba mchana kweupee, aomba msaada kwa RC Makonda (Video)

Mama mmoja mkazi wa Kariakoo jijini Dar es salaam amejikuta katika wakati mgumu baada ya nyumba yao ya urithi iliyopo katika kiwanja namba 10 Kitalu namba 38 Mtaa wa Sukuma Kariakoo Ilala Jijini Dar es salaam kupigwa mnada na mfanyabiashara ambaye alidai aliingia naye ubia wa kujenga ghorofa katika kiwanja hicho halafu wagawane floor.

Mama huyo ambaye alijitambulisha kwa jina, Uwenacho Salum, alisema baada ya kesi yao ya mirathi ya ndugu zake kumalizika Mahakamani, kuna ndugu yao mmoja ambaye alitaka kupewa sehemu ya mirathi hiyo, ndipo walipohamua kumtafura mtu ambaye ataweza kujenga jengo la ghorofa 8 halafu wagawane floor, pamoja na kumlipa ndugu yao humo moja sehemu ya mali yake, lakini mambo yakawa tofauti walivyokubaliana na mwekezaji huyo.

Kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni udalali Unyangala Auction Mart, Patric Sanga ameiambia Bongo5 kwamba ni kweli kampuni yake imepiga mnada nyumba hiyo baada ya kupewa kazi hiyo na Mahakama ya mwanzo Kariakoo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents