Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mama Diamond alinipigia simu nirudiane na mtoto wake, tatizo mawifi – Hamisi Mobetto

Mwanamitindo Hamisa Mobetto Ijumaa hii amefunguka kuzungumzia mahusiano yake ya familia ya baba mtoto wake, Diamond Platnumz.

Hamisa Mobetto, Mama Diamond pamoja na mdogo wake Diamond, Esma

Akizungumza na The Playlist Ijumaa hii, Hamisa amedai kwamba mama Diamond alimpigia simu akimtaka arudiane na mtoto wake.

“Mama Diamond alinipigia simu nirudiane na Diamond, lakini mawifi ndio hivyo tena,” alisema Mobetto kupitia interview hiyo.

Aliongeza, “Diamond hajielewi, nimem-block insta ya mtoto kwa sababu anashindwa hata kujisitiri, hadi anamuhusisha mtoto kwenye mambo yake, nakosa deal kibao za mtoto kisa mambo yake,”

Wiki chache zilizopita mrembo huyo ambaye kwa sasa ameingia kwenye muziki alikumbwa na kashfa nzito ya kumroga baba wa mtoto wake Diamond baada ya kusambaa sauti yake mtandaoni akizungumza na mtu anayedaiwa kuwa ni mganga wa kuenyeji.

“Sauti ilikuwa ya kwangu, hakuwa ni mganga alikuwa ni Sheikh kwaajili ya dua, ni vitu vya kawaida sana lakini walirekodi,” alisema Hamisa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW