Burudani

Mama mzazi wa Hisia awaomba Watanzania kumpigia kura mwanae aibuke mshindi wa TPF6

Mama mzazi wa mshiriki wa Tusker Project Fame Mtanzania Elisha Hisia Simon, amewaomba watanzania kuendelea kumpigia kura mwanae ili awe mshindi wa mwaka huu wa shindano hilo.

1450935_583427941727748_274397649_n

Mama Hisia pia amewaasa wazazi kuwapa fursa watoto wao wanapoonesha nia ya kufanya jambo fulani kulingana na vipaji vyao kwani ni njia pekee ya kuwatengenezea maisha ya kujiamini, kutokata tamaa na kujitambua.

Akiongea na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM , Mbeya, Mama Hisia ameweka wazi namna ambavyo amekuwa akimsaidia mwanae kufanya muziki kutokana na kuipenda fani hiyo kwa muda mrefu na amedai muziki sio uhuni kama inavyodhaniwa na wazazi wengine.

Amesema iwapo mzazi ukimkatalia mtoto kufanya awezalo, unaweza kumharibia vitu vizuri ambavyo wangeweza kuvifanya na kuwaingizia kipato.

“Mimi naamini sana katika uwezo wa kila mtu na kwamba kila mtu akiwezeshwa katika lile ajambo ambalo analiweza atalifanya vizuri. Muziki sio uhuni muziki ni fani, uhuni ni tabia. Kwahiyo mimi mtoto wangu alipoonesha nia ya kuweza muziki na ndugu zake wanaweza vitu vingine na wao najaribu kuwasaidia katika eneo ambalo wanafikiri kwamba ndilo litakaloendesha maisha yao kwa hiyo kama mzazi msaidie juu ya mwanao ukiona anapenda hesabu msaidie hesabu na ukiona anajiweza katika sanaa msaidie katika sanaa,” alisema.

Katika hatua nyingine Mama Hisia alimwelezea mwanae alikoanzia muziki.

“Mwanangu HISIA amesoma Shule ya msingi Nchini Uingereza nilikuwa huko mimi kusoma, sasa kule alikuwa ameanza kuimba jukwaani mapema tu akiwa darasa la tatu au la nne nafikiri, kwa hiyo alipata nguvu sana akiwa kule alikuwa anang’ang’ania na kujiamini alikuwa mzuri sana jukwaani kuliko hata sasa lakini tulipokuwa nyumbani(Tanzania) tulikuwa tunampeleka tuition fulani fulani hapa za lugha. Muziki haikutosha sana baadae alipomaliza kidato cha sita akafanya ya muda mrefu kidogo nyumbani kuagiza vifaa kutoka nchi nyingine walizoendelea akawa anajizoesha nyumbani na kuna wakati tukaenda Dar es salaam akaungana na wenzake ambao ni producers imemsaidia kwa hiyo umeona jinsi anavyofuatilia ni kitu ambacho kipo kwenye moyo wa mtu.”

HISIA anategemea kura zako ili ashinde. Kumpigia kura ingia hapa https://tusker.mobi/register (kura moja kwa siku) au tuma SMS yenye neon Tusker12 kwenda namba 15324(SMS 5 kwa mtu mmoja kwa siku.).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents