Michezo

Mama wa Andy Murray amkingia kifua mwanae

Mama mzazi wa mchezaji tennis, Andy Murray anaefahamika kwa jina la Judy amesema kuwa kijana wake hajakata tamaa kwenye tasnia hiyo na hivyo anafanya kilakitu kuhakikisha anakuwa fiti.

Bingwa huyo mara mbili wa michuano ya Wimbledon amekuwa nje ya uwanja tangu mwaka jana baada ya kufanyia upasuaji mwezi Januari.

Mama wastaa huyo, Judy amesisitiza kuwa kijana wake mwenye umri wa miaka 30, yupo tayari kwa michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kuanza Julai 2.

“Lengo lake muda wote ni kuwa tayari na msimu, nina hakika endapo atakuwa na habari yoyote  ataeleza.” Judy Murray amekiambia chombo cha habari cha BBC.

Mama huyo alipo ulizwa na wanahabari kama anahofia juu ya tasnia ya mwanae kufikia mwisho amesema kuwa kamwe hafikiri hicho kitu kwakuwa Murray anapata kila anachokihitaji katika kuhakikisha anapiga hatua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents