Habari

Mama wa Marekani atarajia kumzaa mjukuu wake, ni baada ya kubeba ujauzito wa binti yake (Gestational Surrogate)

Mwanamke mwenye miaka 58 wa huko Utah nchini Marekani anatarajia kumzaa mjukuu wake wa kwanza.

2e18de84246b5a01480f6a706700729a
Mama na mwana

Julia Navarro anabeba ujauzito wa binti yake, ‘gestational surrogate’ (Mwanamke anayewasaidia wanandoa/wapenzi kupata mtoto kwa kubeba kiini cha mimba (embryo) kilichotengenezwa na watu hao na kisha kuhamishiwa kwenye tumbo lake la uzazi).

Hiyo ni baada ya binti yake na mumewe kuwa na matatizo ya kushika mimba. Binti wa Navarro, Lorena McKinnon alisema alianza kujaribu kutafuta mtoto na mumewe Micah McKinnon, miaka mitatu iliyopita.Msichana huyo mwenye miaka 32 anayeishi katika mjini wa Provo anasema mimba zake nyingi zimekuwa zikitoka huku ujauzito uliokaa kwa muda mrefu ni ule uliodumu kwa wiki 10.

006305a8246d5a01480f6a706700172c

Baada ya majaribio kadhaa, wapenzi hao wakaanza kutafuta mtu wa kubeba mimba yao. McKinnon alisema rafiki yake pamoja na dada yake walikuwa wamekubali kuubeba lakini yeye alikataa. Hapo ndipo mama yake alipoamua kujitolea.

“Kama familia, tunatakiwa kusaidia” Navarro aliliambia gazeti la The Salt Lake Tribune.
7457a38c24705a01480f6a706700c155

Navarro alitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa hormone kwa miezi mitatu kabla ya kiini kilichorutubishwa na mume wa mwanae kupandikizwa. Kutokana na umri wake, madaktari walionya kuwa kulikuwa na asilimia 45 tu kwa zoezi hilo kufanikiwa.Lakini zoezi lilifanikiwa na Navarro ameendelea kuubeba ujauzito huo bila shida.

Hata hivyo kabla ya uamuzi huo, wanandoa hao pamoja na Navarro walihitaji miezi mitatu ya ushauri nasaha. “Wanasaikolojia walitaka kuhakikisha kuwa tunajua tunachoenda kukifanya kwamba tumejiandaa kiakili,” alisema,
McKinnon.”Mara nyingi watu wanaobeba mimba ni watu usiowafahamu. Ni ajabu kuwa na mkataba na mama yangu.”

Kwa mujibu wa sheria za Utah, surrogates wanatakiwa kuwa na miaka zaidi ya 21, wenye kipato kizuri na lazima wawe wamezaa. Wapenzi wanatakiwa kuwa wamefunga ndoa na wanatakiwa kutoa fedha ya kutosha kumlipa mbebaji.

Kwa kawaida, wanandoa hutumia kama dola $60,000 (takriban shilingi milioni 1) katika mchakato huo lakini uamuzi wa mama McKinnon kuibeba mimba hiyo imewasaidia kupunguza karibu nusu ya gharama zake.

Mtoto huyo wa kike anatarajia kuzaliwa mwezi ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents