Michezo

Mamake Paul Pogba ateuliwa kuwa balozi wa soka la wanawake

Shirikisho la soka nchini Guinea (Feguifoot) limemchagua mamake kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba kuwa balozi wa soka la wanawake.

Uteuzi wa Yeo Moriba unajiri baada ya mkutano na rais wa shirikisho hilo Mamadou Antonio Souare.

Souare anatumai kwamba mchezaji huyo wa Ufaransa Paul na nduguze, Florentin na Mathias, watamsaidia mama yao katika jukumu hilo jipya.

Moriba amewahi kuichezea timu ya soka ya wanawake nchini Guinea.

”Najivunia kile ambacho shirikisho la soka la Guinea na rais wake limefanya”, aliambia tovuti ya Feguifoot.

Florentin na Mathias ambao wote walizaliwa nchini Guinea wameichezea timu ya taifa ya Guinea Syli Nationale, kabla ya Moriba kuhamia Ufaransa ambako Pogba alizaliwa.

Beki Florentin mara ya mwisho alichezea klabu ya Genclerbirligi. Huku Naye mshambuliaji Mathias akiendelea kuichezea klabu ya Ufaransa Tours.

Matumaini ni kwamba familia hiyo itafanikiwa kuimarisha hadhi ya soka ya wanawake nchini Guinea.

Ikilinganishwa na wenzao wanaume, timu hiyo ya wanaume haijawahi kufuzu katika kombe la Afrika, kombe la dunia ama hata michezo ya Olimpiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents