Habari

Mamalaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) yataja mikoa 5 yenye tahadhari ya kukumbwa na mvua Upepo mkubwa

Mamalaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) yataja mikoa 5 yenye tahadhari ya kukumbwa na mvua Upepo mkubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, DSM, Zanzibar na Pwani kwa muda wa siku tano kuanzia jana, athari zinazoweza kutokea ni pamoja na Makazi kuzungukwa na maji na ucheleweshwaji wa usafiri.

Mkoani Mtwara tayari mvua kubwa imeanza kunyesha ambapo Uongozi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani umewataka wakazi wake wote wanaoishi mabondeni kuhama mara moja.


Lakini taarifa kutoka Manispaa ya Mtwara zinasema “Kuna Wakazi wamejenga sehemu hatarishi na Halmashauri ilishawapa taarifa ya kuhama na kuwekewa alama ya bomoa ila wameonekana kukaidi na wengine hata kufuta alama za kubomoa zilizowekwa katika nyumba zao, mvua zimeanza majanga yakitokea tusitafute Mchawi”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents